CHADEMA YALAANI MATUKIO YA WATU KUTEKWA
Na TImothy Itembe, Tarime
CHAMA cha Demokorasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulilana.
Akizungumza kwenye mkutano wa Uchaguzi wa viongozi wa CHADEMA Jimbo la Tarime Mjini Januari, 5, 2024, Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mara, Lucas Ngoto alisema wanalaani matukio ya watu kutekwa na wasio julikana na kusababisha familia zikitaabika.
Mwenyekiti huyo amezitaka mamlaka husika kuchukua hatua kukomesha matukio hayo kwa kile alichoeleza kuwa wanaotekwa ni raia wema na hawana hatia na endapo wanashukiwa kwa kujihusisha na vitende vya kihalifu hatua za kisheria zichukuliwe.
"Kumekuwepo na matukio ya hapa na pale ya watu kutekwa na kupelekwa kusiko julikana, matukio kama hayo sisi CHADEMA tunayalaani na tunaomba mamlaka husika kuchukua hatua ya kuyakomesha"alisema Ngoto.
Naye Mwenyekiti wa Jimbo la Tarime mjini, Selemani Abdala maarufu SAUTI wakati anajiuzulu nafasi yake kabla ya kuchaguliwa tena kushika kiti hicho alisema Chama cha Demokorasia na Maendeleo kimejiimarisha kisiasa Jimbo la Tarime mjini.
Ameongeza kusema kuwa kimejipanga katika chaguzi zinazokuja na kwamba kinachosubiriwa ni kipenga cha uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 ili kukomboa nafasi zote zitakazokuwa zikiwaniwa kwenye mitaa,vitongoji na vijiji.
Post a Comment