HEADER AD

HEADER AD

RUWASA YAFIKISHA MAJI KATA 23, KATI YA KATA 26 TARIME VIJIJIJI


Na Dinna Maningo, Tarime


KATA 23 kati ya kata 26 Katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime, mkoani Mara zimefanikiwa kupata maji ambapo kata 3 pekee ndio hazijafikiwa na mradi wa maji na kwamba kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 kata zilizosalia zitakuwa zimepata maji.

Akizungunza na DIMA Online, Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Masheku Malando amesema kuwa Kata ambazo hazijafikiwa na mradi wa maji katika halmashauri ya wilaya ya Tarime ni Kata ya Mbogi, Bumera na Pemba.

Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Nazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Masheku Malando 

Meneja huyo ameyasema hayo wakati alipohojiwa na gazeti hili kuhusu malalamiko ya Diwani wa Kata ya Muriba Mniko Msabi Mariba kudai kuwa Kijiji cha Bungurere hakijafikiwa na mradi wa maji jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi wake.

"Diwani analalamika bure kata yake imefikiwa na mradi, vijiji vimepata maji isipokuwa kijiji cha Bungurere. Kila kitu kinatekelezwa kwa bajeti kwa jinsi tunavyopokea fedha kutoka serikalini.

"Bora yeye kata yake imefikiwa na mradi wa maji kuna kata tatu hazijapata maji kabisa, kwa sasa tunadili na kata tatu ambazo hazina maji kabisa, tageti yetu kila Kata ipate maji kabla ya uchaguzi mkuu wa 2025 " amesema Malando.

Hivi Karibuni katika Maadhimisho ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM, Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara iliadhimisha kuzaliwa kwa CCM katika Kata ya Muriba ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara Julius Masubo.

Katika Maadhimisho hayo Diwani huyo wa Kata ya Muriba alikieleza chama kuwa Kijiji cha Bungurere hakijafikiwa na mradi wa maji jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wananchi.



No comments