HEADER AD

HEADER AD

WATENDAJI WA MAHAKAMA WATAKIWA KUTENDA HAKI KWA WAKATI


Na Thimothy Itembe, Tarime

WATENDAJI wa Mahakama wilayani Tarime mkoa wa Mara, wametakiwa kutenda haki na kwa wakati pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao kwa wateja.

Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Tarime mkoani Mara, Simbanilo Changila ambaye ni mkuu wa Divisheni ya elimu sekondari, halmashauri ya mji wa Tarime wakati wa kilele cha wiki ya sheria inayoadhimishwa kila Februari, 1, ya kila mwaka.


Afisa huyo amesema serikali imewaamini watumishi wa mahakama hivyo wanapaswa kusimama katika haki kwa kuzingatia sheria katika uendeshaji wa kesi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Veronica Selemani amesema mnyororo wa haki jinai unakubwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ile ya mifumo katika taasisi hizo kutokusomana na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa utoaji haki.

     
Hakimu huyo ameomba mfumo kuboreshwa kwenye taasisi kama vile taasisi za upelelezi wa makosa ya jinai (TAKUKURU), mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali kitengo cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya.

Pia kuunganisha mifumo jumuishi ya upelelezi, uchunguzi iliyopo sasa katika taasisi mbalimbali ili kurahisisha utoaji wa haki jinai.

"Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali ifanye jitihada za kuandaa miswaada yenye kuakisi mabadiliko ya sheria yenye lengo la kuondoa vikwazo vya upatikanaji haki jumuishi.

"Bunge lifanyie marekebisho ya sheria zinazozuia upatikanaji wa haki jumuishi pale miswaada ya mabadiliko inapofika bungeni"amesema Veronica.

Naye Wakili wa serikali Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Tawabu Yahaya Issa akisoma taarifa kwa niaba ya Naibu ya Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Mwanasherua mkuu wa Serikali amesema;


" Kwa mjibu wa ibara ya 107A(1) ya katiba ya jamuhuri ya muungamo wa Tanzania ya mwaka 1977 mamlaka ya mwisho'' ya utoaji haki katika jamuhuri ya muungano yamewekwa chini ya mahakama ya Tanzania.

" Hata hivyo mahakama pekee haiwezi kufanikisha jukumu hilo bila kushirikiana na wadau wengine" amesema.

Mwanasheria huyo ameongeza kuwa  wadau wana haki katika sekta ya umma na sekta binafsi na wananafasi kubwa na muhimu katika kuisaidia mahakama kutekeleza jukumu lake la utoaji haki ambayo ni nguzo muhimu kwa ustawi wa Taifa.

Amesema utoaji haki utafanikiwa iwapo wadau wote wa mahakama watashirikiana .





No comments