MAHAKAMA TARIME YAIOMBA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKUMBA MNYORORO WA HAKI JINAI
Na Dinna Maningo, Tarime
HAKIMU Mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Tarime mkoani Mara, Veronica Selemani amesema Mnyororo wa haki jinai unakubwa na changamoto mbalimba ikiwemo mfumo katika taasisi kutosomana.Ameyasema hayo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambayo hufanyika kila mwaka ya Februari, 1, ambayo ni kiashiria cha kuanza mwaja mpya wa kimahakana.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya wilaya ya Tarime, Veronica Selemani
Taasisi zingine ni Kitengo cha kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kuunganisha mifumo jumuishi ya upelelezi/ uchunguzi iliyopo sasa katika taasisi mbalimbali ili kuharakisha utoaji wa haki jinai
Hakimu Veronica ameiomba serikali kupitia Polisi na taasisi zingine za uchunguzi kuanzisha mfumo wa jumuishi wa TEHAMA utakaosaidia kufuatilia mienendo ya vielelezo mahakamani.
Pia uondoshaji wa vielelezo hivyo, mathalani, kusomana kwa mfumo wa uchukuaji, upokeaji, uhifadhi, utoaji wa vielelezo mahakamani na uondishaji wake kati ya jeshi la polisi, ofisi ya Taifa ya mashtaka na mahakama.
Amesema pia kuna haja ya mawakili wa serikali na wa kujitegemea kujenga uhusiano ili kufikia malengo ya usikilizwaji wa mashauri kwa njia ya mtandao.
Amesema ni vyema ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali kufanya jitihada za kuandaa miswada yenye kuakisi mabadiliko ya sheria yenye lengo la kuondoa vikwazo vya upatikanaji haki jumuishi.
Hakimu Veronica ameliomba bunge kufanya marekebisho ya sheria zinazozuia upatikanaji wa haki jumuishi pale miswada ya mabadiliko inapofika bungeni.
Vile vile Wizara ya fedha iziwezeshe taasisi za haki jinai kutimiza majukumu yake kwa kutenga bajeti inayotosheleza majukumu ya taasisi za haki jinai.
Amesema mahakama na wadau wote wa haki jinai katika wilaya ya Tarime watashirikiana kwa pamoja kufanikisha nguzo ya pili na ya tatu ya mpango mkakati wa mahakama kama kauli mbiu isemavyo;
" Umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa jamii wa Taifa; Nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi wa haki jinai.
Post a Comment