HEADER AD

HEADER AD

BLACK SIX YAICHAPA KIDULI FC DAKIKA YA 47

Na Gustafu Haule, Pwani

MASHINDANO ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa yameanza kutimua vumbi Machi 8, mwaka huu katika viwanja vya Tamco vilivyopo Mjini Kibaha kwa kuzikutanisha timu ya  Kiduli FC  na Black Six ya Jijini Dar es Salaam .

Katika mchezo huo Black Six wameibuka na ushindi wa bao 1-0  lililofungwa katika dakika 41 ya  kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wao Kelvin madalisto aliyefunga kupitia mpira wa kichwa uliopigwa kutoka kulia mwa dimba hilo.

Kocha wa Kiduli FC Hery Kisanga , amesema kuwa mchezo wao wa kwanza wamefungwa kutokana na makosa yaliyofanywa na wachezaji wake lakini kufungwa kwao hakuwafanyi kukata tamaa .

      Kocha wa timu ya Kiduli FC Hery Kisanga akizungumza na  waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao na timu ya Black Six uliopigwa Machi 8  katika viwanja vya Tamco Kibaha

Kisanga amesema kuwa kwa sasa wanajipanga na michezo mingine inayofuata na watakwenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza na ana imani michezo ijayo itakwenda kuzaa matunda.

"Leo tumefungua mashindano haya lakini tumekubali kupoteza mchezo huu lakini tunaenda kuyafanyiakazi mapungufu yaliyojitokeza na tunaimani tutafanya vizuri,"amesema Kisanga" amesema.

    Wachezaji wa timu ya Kiduli FC na Black Six wakiwa katika michuano ya ligi ya mabingwa.

Kisanga amewaomba washabiki wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi katika kuisapoti timu yao pale inapocheza ili hiweze kupata nguvu ya ushindi wa michezo mingine ijayo.

Kocha wa Black Six Omary Mbweze, amesema siri ya ushindi wao ni wachezaji wake kujituma na kutumia vizuri nafasi waliyopata huku akiongoza kuwa ushindi huo umewapa nguvu ya kupambana na michezo mingine ijayo.

Kocha wa timu ya Black Six Omary Mbweze akiwaeleza Waandishi wa habari siri ya ushindi wa timu yake baada ya kuifunga Kiduli FC bao 1-0.

Hata hivyo kituo cha mkoa wa Pwani  kimejumuisha timu zote zilizopangwa kundi B ikiwemo Singida Cluster, Black Six,Moro Kids, Stand FC, Red Angels,Gunners FC, na wenyeji Kiduli FC.



No comments