TRA KAGERA YAKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 30 NDANI YA MIEZI MITATU
Na Alodia Babara, Bukoba
MAMLAKA ya Mapato Tanzania ( TRA) mkoa wa Kagera imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato ambapo katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024 imekusanya Tsh. Bilioni 30.2 sawa na asilimia 107.
Meneja wa mamlaka hiyo mkoa wa Kagera Castro John ameyasema hayo wakati akizumgumza na waandishi wa habari Aprili 25, 2024 katika kikao kilicholenga kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari pamoja na kueleza mafanikio ya ukusanyaji wa kodi kipindi cha Januari hadi Machi, 2024.
"Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoa wa Kagera tulipanga kukusanya Tsh. Bilioni 28.24 lakini tulikusanya Tsh. Bilioni 30.2 na hivyo kuvuka lengo na kufikia asilimia 107" amesema Castro.
Castro ametolea ufafanuzi wa kodi mpya ya bodaboda ambayo inapaswa kulipwa kwa mwaka elfu 65,000 ambapo kila robo mwaka inapaswa kilipwa Tsh. 16,200 na zinalipwa kwa awamu nne hivyo amewomba wamiliki wa pikipiki za biashara kulipa kodi hiyo.
Aidha katika mkutano huo amewaomba Waandishi wa habari kuendelea kuhamasisha walipakodi kulipa kwa wakati ili kuongeza mapato ya nchi.
Afisa Elimu kwa Umma Ruekaza Rwegoshola ameeleza kuwa, kipitia ulipaji kodi serikali imekuwa ikitoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake zikiwemo huduma za Afya, maji, ujenzi wa miundombinu ya barabara na vyumba vya madarasa.
Ameongeza kuwa asilimia 70 ya mapato ya serikali yanatokana na ukusanyaji kodi na kwa mwaka 2023/2024 serikali ilipitisha bajeti ya trioni 44.39 na TRA ilipewa lengo la kukusanya trioni 26.75 hivyo TRA inayo kazi kubwa kuhakikisha inakusanya kodi.
Post a Comment