DC MASWA AKABIDHI PIKIPIKI KWA WATOA HUDUMA YA MAJI NGAZI YA JAMII
Na Samwel Mwanga, Maswa
MKUU wa wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, Aswege Kaminyoge amekabidhi pikipiki nne aina ya TVS 150 kwa watoa huduma ya maji ngazi ya Jamii (CBWSO) Isulilo-Ilamata , Nguliguli na Mwabulimbu wilayani humo ili kurahisisha kutoa huduma kwenye maeneo ya vijiji wanavyovihudumia.
Pikipiki hizo zimenunuliwa na Mkandarasi M/SEPIC LTD aliyekuwa akitekeleza ujenzi wa mradi wa maji Kadoto na Kinamwigulu ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kipengere cha ununuzi wa pikipiki mbili katika kila mradi.
Pikipiki nne aina ya TVS 150 zilizonunuliwa na Ruwasa wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu zilizotolewa kwa Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) za Isulilo-Ilamata ,Nguliguli na Mwabulimbu.Pikipiki hizo ni za thamani ya Tsh. Milioni 16.6 chini ya mradi wa lipa kwa matokeo (Pfor R) ambao ni program ya maji chini ya mkopo wa benki ya Dunia.
Akikabidhi pikipiki hizo Mei, 7 mwaka huu kwenye viwanja wa ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dc Kaminyoge amesema huduma ya upatikanaji wa maji katika wilaya ya Maswa imegawanyika katika maeneo mawili ya mjini na vijijini kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge(mwenye suti rangi ya ugoro)akiwasha Moja ya pikipiki zilizonunuliwa na Ruwasa kwa ajili ya CBWSOAmesema kuwa kwa upande wa vijijini, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata maji kupitia miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu ambaye amekuwa akitoa fedha katika kutekeleza miradi hiyo iliyoko wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu, Aswege Kaminyoge akijaribu pikipiki aina ya TVS 150 ambazo zimetolewa na Ruwasa kwa ajili ya Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) za Isulilo-Ilamata , Nguliguli na Mwabulimbu zilizoko wilayani humo.Amesema lengo la kukabidhi pikipiki hizo ni kurahisisha kufika kwenye eneo lenye changamoto ya maji kwa haraka na kuitatua ukizingatia kila jumuiya ina eneo kubwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi katika vijiji vyao na zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Pikipiki zote zilizokabidhiwa zifanye kazi iliyokusudiwa ya huduma ya maji kwa wananchi zisiwe za kubeba abiria wala mizigo na wewe uliyekabidhiwa pikipiki elewa ni mali ya mradi ni ya CBWSO).
"Yeyote katika ile kamati akitaka pikipiki kwa ajili ya kutumia kwenye shughuli ya maji aweze kuitumia na wewe uliyekabidhiwa ni kwa ajili ya kuitunza na usajili wa pikipiki hizi usajili ufanyike kwa namba za serikali ili zijulikane zinapokwenda kufanya kazi za serikali,”amesema.
Pia amwasihi kuzitunza ili zidumu kwa muda mrefu na kuhakikisha kuwa lengo la serikali linafikiwa la utoaji wa huduma ya maji kwa maeneo ya vijijini inafikia asiliamia 85 hadi kufikia mwaka 2025 kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ya mwaka 2020 hadi 2025.
Ameongeza kuwa RUWASA iendelee kuvisaidia Vyombo vya Watoa Huduma ya Maji ngazi ya jamii kwa kuwa vilivyo vingi bado havina uwezo wa kujitegemea kutokana na kutokuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya kujiendesha sambamba na kutoa elimu katika miradi ya maji hasa katika suala la uendeshaji.
Awali Afisa Maendeleo RUWASA wilaya ya Maswa, Wilson Magaigwa amesema kuwa vyombo hivyo vya watumiaji Maji ngazi ya jamii (CBWSOs) vimekuwa vikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uhaba wa vyombo vya usafiri kwani maeneo ya utekelezaji ni makubwa sana.
Afisa Maendeleo Ruwasa wilaya ya Maswa,Wilson Magaigwa(aliyeko mbele)akisoma taarifa ya hali ya upatikanaji wa Maji Vijiji wilayani humo kwa Mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge(mwenye suti rangi ya ugoro)“CBWSOs moja katika wilaya ya Maswa inaweza kuhudumia zaidi ya kijiji kimoja huku akitolea mfano kwa CBWSOs za Nguliguli ina vijiji vitano na Isulilo-Ilamata ina vijiji kumi hivyo kusababisha wakati mwingine utendaji wa Vyombo hivyo kushuka,”amesema.
Amesema kuwa changamoto ya utatuzi wa usafiri kwa CBWSOs ni kuweka katika kila bajeti ya kununua vyombo vya usafirikupitia kwenye miradi ya maji vijijini kadri itakavyoendelea kujengwa.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA wilaya ya Maswa, Mhandisi Lucas Madaha amesema kuwa kwa kipindi cha miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Sukuhu wilaya hiyo wameweza kuongeza upatikanaji wa maji vijijini kutoka Ailimia 68.9 kwa mwaka 2019 na kwa sasa wamefikia asilimia 74.6 hadi sasa.
“Tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuiwezesha RUWASA kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji Vijijini.
"Katika miaka hii mitatu ya uongozi wake kwa wilaya ya Maswa tumeweza kuongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 68.9 kwa mwaka 2019 na hadi sasa tumefikia asilimia 74.6 kwa maeneo ya vijijini’”amesema
Naye Msimamizi wa CBWSO ya Shishiyu, Stephen Biseko amemwahidi mkuu wa wilaya kuitumia pikipiki hizo kwa lengo lililohitajika hivyo kuwahaidi wananchi kutoa taarifa ya changamoto pindi inapotokea kwenye vijiji vyote vilivyoko kwenye maeneo yao ili waweze kutatua changamoto za upatikanaji wa maji kwa wananchi katika maeneo yao.
Post a Comment