RC KAGERA : AVIPONGEZA VIJIJI VILIVYOTOA ENEO UJENZI TAWI LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
Na Alodia Babara, Bukoba
MKUU wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa ametaja manufaa manne yatakayopatikana baada ya kukamilika ujenzi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam ikiwemo kupanua mji, kukuza uchumi, kuongeza fulsa kwa vijana wa Kagera na kuongeza urafiki.
Tawi hilo la chuo kikuu litajengwa katika kijiji cha Itahwa kata ya Kalabagaine halmashauri ya Bukoba na eneo la chuo hicho ni hekali 315 ambazo zilitolewa na wananchi wa vijiji viwili vya Kangabusharo na Itahwa na hafla ya kukabidhi eneo la ujenzi kwa mkandarasi imefanyika Mei 29,mwaka huu.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa akiwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika eneo litakapojengwa tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam amewashukuru wananchi kwa kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na kutoa manufaa manne yatakayopatikana baada ya kukamilika kwake.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Fatma Mwassa akizungumza na wananchi katika hafla ya kukabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa mradi wa tawi la chuo kikuu cha Dar es Salaam kitakachojengwa kijiji cha Itahwa kata ya Kalabagaine halmashauri ya Bukoba"Nitumie nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutukumbuka wanakagera kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu, wanakagera walitamani kuwa na chuo kikuu miaka mingi iliyopita kwani wanahistoria ya kupenda kusoma .Niwapongeze wananchi wa vijiji viwili kwa kutoa eneo kujenga chuo kikuu" amesema Mwassa
Ameongeza kuwa wanatambua chuo hicho ni kwa ajili ya watanzania wote na raia wa nchi nyingine lakini watatumia fulsa hiyo vizuri.
Amesema kuwa, uwepo wa mradi huo utaleta fulsa mbalimbali kwa wakazi wa mkoa wa Kagera ikiwemo fulsa ya elimu kwa wakazi wa Kagera kwani kitakuwepo kituo cha mafunzo ya ujasiriamali hata kama mtu hajamaliza kidato cha sita, kupanua mji, kukuza uchumi, na kuongeza urafiki.
Aidha ametoa Rai kwa wanafunzi wanaosoma shule za sekondari zinazozunguka eneo la chuo kikuu kuongeza bidii katika masomo ili watakapohitimu kidato cha sita waweze kuendelea na masomo ya juu katika chuo hicho.
Pia amemtaka mkandarasi wa ujenzi katika chuo hicho kumaliza kwa wakati ujenzi huo
Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayeshughulikia taaluma Prof. Beneventura Rutinwa amesema mpango wa ujenzi wa tawi la chuo hicho ulianza mwaka 2019 na kwa kipindi cha kwanza cha ujenzi zitatumika Tsh. Bilioni 20.
Amesema ujenzi ulianza Mei 17,2014 utakamilika Octoba mwaka kesho utachukua muda wa miezi 18.
Aidha mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema, wilaya iko tayari kutoa ushirikiano kipindi chote cha utekelezaji wa ujenzi huo.
Post a Comment