IBADA YA WATU WENYE ULEMAVU YAWAVUTIA VIONGOZI WA KISABATO JIMBO LA MARA
Wakizungumza katika ibada hiyo siku ya jumamos, Agosti, 3, 2024 iliyoendeshwa na watu wenye ulemavu wa viungo, Askofu wa jimbo kuu la Mara, Mchungaji Joseph Matongo amesema kuwa ni mara ya kwanza katika jimbo l Mara ibada kuendeshwa na watu wenye ulemavu wa viungo ambapo pia wanaendesha mahubiri ya injili wiki tatu yaliyoanza jumapili katika viwanja vya shule ya msingi Nyamongo ambayo yatahitimishwa Agosti , 24, 2024.
Aidha, Askofu huyo pamoja na Katibu mkuu Benjamini Ngarama na Mhazini mkuu Padon Kikiwa wa jimbo kuu la Mara, wamempongeza Katibu wa idara ya watu wenye ulemavu Kanisa la Nyamongo Kati, Bhoke Orindo mwenye ulemavu wa macho kwa kuwaunganisha watu wenye walemavu wa viungo mkoani Mara kushiriki ibada pamoja na kuwa na maono ya kuendesha mahubiri.
Mahubiri hayo yamefadhiliwa na Charles Mseti pamoja na Joshua Mrimi wakazi wa Dar es Salaam waliochangia Tsh. Milioni 10 kufadhili mahubiri ambapo washiriki wa Nyamongo Kati wamechangia Tsh. Milioni tano.
Tukio
la watu wenye ulemavu kuendesha mahubiri ya injiri limewavutia viongozi wa
jimbo la Mara na hivyo jimbo kuchangia Tsh. laki tano kuunga mkono jitihada za
watu wenye ulemavu katika kufanikisha mahubiri.
Post a Comment