HEADER AD

HEADER AD

MWALIMU MAHAKAMANI KWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI

Samwel Mwanga, Itilima 

MWALIMU Subiri Andason(37)wa shule ya Sekondari Nguno katika wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya hiyo kujibu shtaka moja la kudaiwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wa kike(17)akiwa nyumbani kwake chumbani.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani Novemba, 10, 2024 katika mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi,Robert Kaanwa na kusomewa shtaka lake hilo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya taifa ya Mashtaka wilaya hiyo,Mkaguzi Msaidizi wa polisi,Jaston Mhule.

Mwendesha Mashtaka huyo ameiezea Mahakama kuwa Mwalimu huyo alitenda kosa hilo, kinyume na kifungu cha 130(1)(2)e na 131(1) cha  sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2022.

Akitoa maeleezo ya kosa hilo, Mhule alieleza kuwa katika kijiji cha Nguno katika eneo la shule ya sekondari Nguno anakofundisha Mshtakiwa alimbaka mhanga ambaye ni mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka 17(jina limehifadhiwa) kwa kufanya nae mapenzi akiwa nyumbani kwake.

     Jengo la Mahakama ya wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu

Ameendelea kwa kueleza kuwa mnamo Oktoba 7 mwaka huu mshtakiwa aliwekwa chini ya ulinzi wa wananchi baada ya kukamatwa akiwa na mhanga chumbani kwake majira ya saa moja usiku na baada ya kumkamata walimfikisha Kituo cha Polisi Wilaya ya Itilima.

Mara baada ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya kosa hilo alikana, ambapo upande wa mashtaka uliwasilisha mbele ya mahakama kuwa ina shahidi mmoja na kusikilizwa huku mshtakiwa akipelekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana.

Hakimu Robert Kaanmwa, alihairisha kesi hiyo mpaka Oktoba 15, 2024 ambapo kesi hiyo itafikishwa mahakamani hapo tena kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

 

 

No comments