HEADER AD

HEADER AD

NYAMBARI NYANGWINE FOUNDATION KUGAWA VITABU SHULE ZOTE ZA SEKONDARI WILAYANI TARIME


>> Ni vitabu vya masomo yote vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 100

>> Msemaji wa Taasisi Jacob Mugini aeleza malengo ya Taasisi

Na Dinna Maningo, Tarime 

ILI Mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yake anahitaji kujisomea vitabu vya ziada na kiada vitakavyomjengea uelewa anapokuwa darasani ama nyumbani.

Kwa kutambua umuhimu wa elimu, Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation (NNF) imenunua vitabu vya masomo mbalimbali vya ziada na kiada vya kidato cha kwanza hadi cha sita vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 100.

Vitabu hivyo vitatolewa bure katika shule zote za sekondani za serikali na za watu binafsi wilayani Tarime, mkoani Mara.

Msemaji wa Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation, Jacob Mugini amewaambia Waandishi wa Habari kwamba tayari vitabu vimewasili wilayani Tarime na vitaanza kusambazwa katika shule zote kuanzia wiki ijayo.

  Msemaji wa Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation, Jacob Mugini akionesha baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Taasisi  

Jacob amesema kuwa msaada huo ni kutokana na maombi ya wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu na Wanafunzi waliyoyatoa kwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Nyambari Nyangwine aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Tarime mwaka 2010-2015.

"Napenda kuwaarifu kuwa Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation (NNF) inatarajia kuanza kutoa msaada wa vitabu wiki ijayo . Mwenyekiti wa Taasisi yupo katika ziara ya kibiashara nje ya nchi katika falme za kiarabu.

" Mwenyekiti Nyambari ameona ni vema kazi ya kugawa vitabu iendelee ili viweze kuwafikia wanufaika mapema kwa kuzingatia kuwa uwekezaji wa sekta ya elimu ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa "amesema Mugini.

" Vitabu ni vya masomo ya Jiografia, Fizikia, Kemia, Uraia, Kiswahili na Bailojia. Asilimia 80 ya vitabu vyote vimeshafika wilayani Tarime " amesema Jacob 

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika shule za Sekondari ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu katika mazingira bora.


" Msaada wa vitabu hivi ni sehemu ya juhudi zinazofanywa na Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation katika kuunga juhudi za serikali kwenye maendeleo ya sekta ya elimu nchini.

" Katika ugawaji wa vitabu shule hazitagharamikia usafiri wa kusafirisha vitabu kuvipeleka shuleni, Taasisi itagharamia usafiri hadi vifike shuleni.

" Nimatumaini yetu kuwa vitabu hivi vitasaidia kutatua au kupunguza changamoto ya vitabu katika shule za Sekondari zilizopo halmashauri ya mji Tarime na Halmashauri ya wilaya ya Tarime " amesema Jacob.

Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation ilianzishwa mwezi, Septemba, 19, 2024 jijini Dar es Salaam ikijikita katika masuala ya maendeleo ya kijamii ikiwemo Elimu, Afya, Maji.

Pi utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini, kumsaidia mtanzania kupiga vita umasikini pamoja kutoa misaada muhimu ya kibinadamu katika maeneo mbalimbali nchini.

             Nyambari Nyangwine ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Nyambari Nyangwine Foundation.





No comments