HEADER AD

HEADER AD

RC KUNENGE AONGOZA MBIO KUHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA

Na Gustaphu Haule, Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwa kuendesha mbio za taratibu za kukimbia (Joging) zenye zaidi ya kilomita 5.

Mbio hizo zimefanyika Mjini Kibaha  leo Oktoba 12 kuanzia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kupitia barabara ya Morogoro na kuelekea Soko la Loliondo na kisha kumalizia katika viwanja vya stendi ya zamani iliyopo Mailimoja Kibaha Mjini.

        Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akikimbia mbio za taratibu (Joging)kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ,Joging hiyo imefanyika Oktoba 12 Mjini Kibaha.

Akizungumza na Wananchi waliokusanyika katika viwanja hivyo Kunenge amesema kuwa lengo la joging hiyo ni kuendelea kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha na hata kupiga kura siku itakapowadia.

Amesema , uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio unaotoa dira ya maendeleo hapa nchini kwakuwa kila jambo linaanza na ngazi za chini na kwamba kujiandikisha kutasaidia kutimiza wajibu na haki ya msingi ya  kuchagua  kiongozi wanayemtaka.

          Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimoni akiendesha burudani ya wasanii katika tamasha la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura Leo Oktoba 12 Mjini Kibaha

"Leo tumefanya joging hii lengo ni kuhamasisha wananchi mjitokeze kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lakini nafurahi kuona hamasa imekuwa kubwa na imani yangu sote tutajiandikisha,"amesema Kunenge

Kunenge amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tayari amejiandikisha Mkoani Dodoma kwahiyo ni vyema na wananchi wa Mkoa wa Pwani wakajitokeza kwa ajili ya kumuunga mkono Rais kwakuwa viongozi watakaochaguliwa ni maslahi ya maendeleo.

      Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akizungumza katika tamasha la michezo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lililofanyika leo Oktoba 12 .

"Nimefarijika kuona umati wa watu waliojitokeza katika Joging hii na kujitokeza huku inaashiria wazi kuwa ndivyo tutakavyojitokeza hata katika vituo vyeti,nendeni mkawahamasishe na wale  waliokuwa nyumbani ili tutimize haki ya kikatiba ", ameongeza Kunenge 

Kunenge,amesema kauli mbiu ya mbio hizo ni "Wananchi wa Mkoa wa Pwani tupo tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa ", huku akisema itakuwa vizuri endapo kila mtu akaitumia kauli mbiu hiyo kwa vitendo.

      Msanii wa nyimbo za Bongofleva Barnaba boy akitumbuiza katika tamasha la michezo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lililofanyika leo Oktoba 12.

Aidha ,katika kutoa hamasa hiyo wasanii mbalimbali walitumbuiza akiwemo Barnaba Boy,Joe Makini na wasanii wengine mbalimbali.

Zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lilianza Oktoba 11 Mkoani Pwani na litafanyika kwa muda wa siku 10 ikiwa mpaka Oktoba 20 huku uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 27 mwaka huu.

        Msanii wa nyimbo za Bongofleva Joe Makini akitumbuiza katika tamasha la michezo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lililofanyika Oktoba 12 Mjini Kibaha.

.    Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt Roger's Shemwelekwa aliyevaa jezi ya Yanga katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge mwenye T-shirt nyeupe (Kulia) katika tamasha la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lililofanyika leo Oktoba 12 katika viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mjini.

No comments