HEADER AD

HEADER AD

RAIS DK. MWINYI : TANZANIA IMEPOKEA WATALII WA KIMATAIFA 2026378

  


Na Andrew Chale, Dar es Salaam 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwa mujibu wa takwimu kutoka sekta ya Utalii, hadi kufikia mwezi Agosti, 2024 zinaonesha kuwa Tanzania imepokea idadi ya watalii wa kimataifa 2,026,378.

Amesema kiwango hicho ni cha juu kabisa kuwahi kufikiwa kwenye historia ya Tanzania na mapato yatokanayo na sekta hiyo, kufikia Dola za kimarekani Tsh. Bilioni 3.5.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo Oktoba,11 2024 kwenye hafla ya ufunguzi wa Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the Swahili International Tourism Expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili (8th edition of the Swahili International Tourism Expo – S!TE 2024) katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam mapema tarehe 11 Oktoba 2024.

Rais Dk.Mwinyi amesema kutokana na juhudi kubwa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan za kukuza utalii nchini, Tanzania imeshuhudia idadi kubwa ya watalii  hao wa kimataifa wanaotembelea sehemu mbalimbali za nchi pamoja na ongezeko la mapato yatokanayo na sekta ya utalii. 

Rais Dk. Mwinyi amebainisha kuwa utalii ni sekta yenye ushindani mkubwa hasa kwa sekta ya utangazaji, bila kutangazwa kimataifa haiwezi kufikia malengo yaliyojiwekea. 




"Mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini kupitia sekta ya utalii yanayoitangaza Tanzania kimataifa na kuitambulisha duniani kuwa nchi ya kwanza Afrika inayofanya vizuri kwa utalii na ya sita dunia nzima.

Mafanikio hayo ni juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha miundombinu ya utalii ikiwemo kuendelea kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).



Amesema pamoja na kuhamasisha mashirika mengine ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na nchi zenye masoko ya utalii, kujenga barabara na reli za kisasa zinazounganisha vivutio vya utalii, kujenga na kukarabati viwanja vya ndege, na kuimarisha huduma nyengine muhimu za utalii." amesema Rais Dk. Mwinyi.




No comments