HEADER AD

HEADER AD

TIMU YA STENDI UNITED SHINYANGA YAZINDUA JEZI MPYA


Na Suzy Butondo, Shinyanga

TIMU ya mpira wa miguu Stendi United ya mkoani Shinyanga  imezindua rasmi jezi mpya za timu hiyo ambazo zitapatikana katika maduka mbalimbali kwa bei ya Tsh. 25,000, zitakazotumika katika msimu wa ligi ya championship 2024/2025.

Msemaji wa Timu hiyo ya Stendi United Ramadhani Zoro, akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo, Agasti, 19,2024 katika uwanja wa nguzo nane manispaa ya Shinyanga.


Amesema jezi hizo zinapatika katika maduka mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine kwa bei ya Tsh.25,000, hivyo amewaomba wanachama wote na wananchi kununua jezi hizo ili kuiunga mkono timu hiyo.

"Niwaombe wanachama wote wa timu ya Stend United, wananchi na wadau wote kuinga mkono timu yetu ili iweze kusonga mbele zaidi na iweze kufikia malengo yake"amesema Zoro.

Kocha Mkuu wa Timu ya Stendi United Meja Abdul Mingange, amewaomba mashabiki wa timu hiyo maarufu chama lawana, kwamba wajitojkeze kwa wingi kuiunga timu hiyo, ili endelee kufanya vizuri katika ligi ya Championship na kuja kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara.


"Kesho tutakuwa na mchezo hapa Shinyanga tukicheza na timu ya Bigmani hivyo tuwaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani ili tupate point 3, na pia tutakuwa na mechi zingine mbili ya Mbeya kwanza na Biashara na tuhitaji kushinda mechi zote ili tupate point 9 na kuendelea kushika nafasi nzuri kwenye ligi hiyo"amesema Mingange.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na usajili wa Timu ya Stendi United Chrispin Kakwaya, amesema jezi hizo mpya zina ubora wa hali ya juu, na kwamba stendi zote nchi nzima timu hiyo ni ya kwao yenye makao yake makuu mkoani Shinyanga hivyo amewaomba watu wote za stend waiunge mkono timu hiyo.


Kapteni wa timu hiyo Babilas Chitembe,amemshukuru mdhamini wa timu hiyo Jambo kwakuendelea kuidhamini, hivyo  amewaomba wananchi wote wajitokeze kwa wingi kununua jezi hizo na kuwasapoti mechi zote wanazocheza ili kuweza kuipandisha timu hiyo iweze kucheza msimu wa ligi kuu tena.

 "Tupo tayari kupambana kwa ajili ya timu hii  ili kuipandisha kushiriki kucheza msimu wa ligi kuu tena, hivyo niwaombe  mashabiki, wanachama, wafanyabiashara  na wadau mbalimbali  watuunge mkono ili kuhakikisha timu hii ya stendi  inapanda"amesema Chitembe.










No comments