HEADER AD

HEADER AD

WENYEVITI WA MITAA WALIOSHINDA KURA ZA MAONI CCM NGAZI YA MATAWI


>> Ni kutoka mitaa 8 Kata ya Turwa 

>> Katibu CCM Turwa asema uchaguzi ulifanyika kwa amani

Na Dinna Maningo, Tarime 

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Turwa Marwa Timoro, amesema jumla ya wanachama 17 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanaotoka Tawi la Mturu, Rebu na uwanja wa Ndege wamejitokeza kuchukua na kurejesha fomu wakitiania ya kugombea nafasi ya uenyekiti wa mitaa ndani ya Kata ya Turwa .

Akizungumza na DIMA ONLINE, Marwa amesema kuwa baada ya kurejesha fomu za kutiania , zoezi la upigaji kura lilifanyika  Oktoba, 23, 2024 katika Matawi hayo. 

Amesema kuwa jumla ya wanachama waliopiga kura katika Matawi yote matatu ndani ya Kata hiyo ni 1273 na washindi walipatikana baada ya kuwazidi kura watiania wenzao na kwamba uchaguzi ulifanyika kwa amani.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Turwa, wilaya ya Tarime, Marwa Timoro

Amesema kilichobaki ni kujadiliwa na kupitishwa katika vikao vya CCM ngazi ya Kata na Wilaya ili kuwapata watakaoipeperusha bendera ya CCM kuchuana na vyama vya upinzani katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba, 27, 2024.

Ametaja majina ya watiania waliochuana na kura walizopata. Katika Tawi la Mturu lenye mitaa mitatu jumla ya wapiga kura walikuwa 620, Mwenyekiti wa mtaa wa Rebu Senta aliyekuwa anatetea nafasi yake hakuwa na mpinzani ameshinda kwa kupata kura 199. 

" Mtaa wa Rebu shuleni watiania walikuwa wawili, aliyeongoza kwa ushindi ni Samson Chuale kura 287 , Macka Marwa kura 12. Mtaa wa Buguti watiania walikuwa wawili. Aliyeibuka mshindi ni John Samweli Chacha (Mboma) kura 102 na John Edward Gairigi kura 20.

" Tawi la Rebu lenye mitaa mitatu lilikuwa na jumla ya wapiga kura 316 kura zingine ziliharibika ambapo mtaa wa Kebikiri watiania walikuwa watatu. 

Mshindi ni Juma Gidion kura 74, Helena D. Waisare kura 11 na James  M.Chacha kura 6. Mtaa wa Gimenya watiania walikuwa wawili ambapo mshindi ni Nashoni Samo kura 92 na Daniel Marwa kura 53 " amesema Marwa.

Mtaa wa Kokehogoma uliokuwa na  watiania  watano mshindi ni Jackson Mbusiro kura 23, Mussa Nehemia kura 13, Methew Petro kura 6 , Tedi James kura 6 na Sabina Segeru kura 2.

Amesema Tawi la Uwanja wa Ndege lenye mitaa miwili wapiga kura walikuwa 337 kura zingine ziliharibika. Mtaa wa Mkuyuni watiania walikuwa wawili. Aliyeibuka mshindi ni Matiko Surati Siong'o kura 39 na Mogosi Magoko Burure kura 18. Mtaa wa Uwanja wa Ndege uliongoza kuwa na watiania saba.

Aliyeongoza kwa ushindi ni Baraka Simion Mwita kura 124 , Joseph Lameck Sahani kura 27, Matiko Joseph Mwikwabe 02, Thobias Joseph Marwa ( Kichichi) kura 7, Bhoke Pius Mwita kura 0, Godfrey John Machingo kura 0 na Waryoba Gaitiryo  Mahende kura 0.

Kwa mujibu wa Tangazo la ratiba ya uchaguzi wa serikali za mitaa iliyotolewa Agosti, 15, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa, kampeni zitaanza Novemba, 20-26,2024 na uchaguzi utafanyka Novemba, 27,2024.

No comments