KESI INAYOMKABILI PADRI NA WENZAKE KWA TUHUMA ZA KUMUUA MTOTO MWENYE UALBINO YAAHIRISHWA
Na Alodia Babara, Bukoba
KESI namba 25513/2024 inayowakabili washtakiwa tisa wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualbino Noela Asimwe Novart imehairishwa hadi Februari, 17, 2025.
Washtakiwa hao wanatuhumiwa kumuua mtoto wa miaka miwili na nusu, mkazi wa Kijiji cha Bulamula kilichoko kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Washitakiwa wa mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualbino Noela Asimwe Novat aliyekuwa mkazi wa kijiji cha Bulamula kilichoko kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera wakiwa mahakamani leo hii.
Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama kuu ya Tanzania, Kanda ya Bukoba, imeahirishwa baada ya mshitakiwa namba moja Padre Elipidius Rwegoshora taarifa zake za kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili kuwa hazijarudi katika mahakama hiyo kutoka Isanga Dodoma
Akizungumza Desemba, 11, 2024, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba, Emanuel Ng'ingwana amesema kuwa, Octoba ,25, mwaka huu walikuwa na ombi la mshitakiwa namba moja Padre Elipidius Rwegoshora (51) kupitia kwa wakili wake Projestus Mulokozi kwamba apelekwe Isanga Dodoma kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake ya akili.
Washitakiwa wa mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualbino Noela Asimwe Novat aliyekuwa mkazi wa kijiji cha Bulamula kilichoko kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera wakiwa mahakamani leo hii
Jaji Emanuel ameongeza kuwa, ombi hilo halikupingwa na mahakama hiyo badala yake mahakama ilitoa amri Padre Elpidius kupelekwa Isanga kwa ajili ya uchunguzi.
Aidha amesema amri ya mahakama ilielekeza apelekwe Isanga na ndani ya siku 42 arudishwe na uchunguzi huo uwe umeishafanyika na taarifa kufungwa.
"Taarifa, Padre Elpidius alipelekwa kwa ajili ya uchunguzi lakini mahakama hii haijapokea taarifa kutoka Isanga juu ya uchunguzi wa afya ya akili, Msajiri anaendelea kufanya mawasiliano maana hata mshitakiwa namba moja hayupo" amesema Jaji Ng'ingwana .
Washtakiwa waliofikishwa mahakamani ni pamoja na Novat Venant (24) baba mzazi wa marehemu Asimwe Novat, dreva bodaboda Nurdin Masoud (25), Ramadhani Selestine (23) Alphonce Rwenyagila (30) pamoja na Faswiu Athuman (39), Gozibert Alkard (35), Desdery Evarist (33), na Dastan Burchard (47).
Ikumbukwe kuwa, Oktoba 25, mwaka huu washtakiwa hao kwa pamoja walifikishwa mbele ya jaji wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Bukoba Emanuel Ng'ingwana aliyekubaliana na maombi yaliyowasilishwa na upande wa jopo la mawakili wa utetezi ya mtuhumiwa namba moja padre Elipidius Rwegoshora kutomsomea mashtaka mshtakiwa yanayomkabili hadi atakapofanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa akili.
Jopo la mawakili wanne wa upande wa utetezi likiongozwa wakili msomi Projestus Mulokozi liliiomba mahakama isitishe zoezi hilo kwa kuwa mteja wao kwa siku hiyo hakuwa na uwezo wa kuongea vizuri pamoja na kuelewa anachokifanya.
Hivyo, asingeweza kujitetea kwa usahihi ,waliomba kupokelewa kwa maombi ya upande wa utetezi yaliyotolewa mahakamani hapo siku hiyo.
Washitakiwa wa mauaji ya kikatili ya mtoto mwenye ualbino Noela Asimwe Novat aliyekuwa mkazi wa kijiji cha Bulamula kilichoko kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera wakiwa mahakamani leo hii.
Aidha mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na wakili wa Serikali mwandamizi, Waziri Magumbo aliyekuwa anashirikiana na mawakili wengine wa serikali, ambao ni pamoja na Erick Mabagala na Matilda Assey hawakuweka pingamizi la aina yoyote walikubaliana na uamuzi uliotolewa na mahakama wa kusitisha zoezi.
Mahakama ilitoa amri mtuhumiwa apelekwe Isanga akapimwe akili hivyo,ilieleza kuwa watuhumiwa wote watasomewa mashtaka ya kesi inayowakabili kwa pamoja baada ya kupatikana matokeo ya uchunguzi wa ugonjwa wa akili wa mtuhumiwa namba moja padre Elipidius Rwegoshora.
Washitakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo Mei 30 mwaka huu katika kijiji cha Bulamula kata ya Kamachumu Wilayani Muleba.
Post a Comment