WASIO NA VYOO SIMIYU KUSAKWA
Na Samwel Mwanga, Maswa
ASILIMIA 38 pekee ya kaya katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu ndizo zina huduma ya choo, hali inayopelekea magonjwa ya mlipuko kutokana na watu kujisaidia sehemu zisizo rasmi.
Mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge amewaagiza viongozi wa wilaya hiyo wakiwemo maofisa afya kuwachukulia hatua watu wote wasio na vyoo kwani kuwa na choo ni jambo la muhimu.
Akizungumza kikao kazi kilichofanyika, Desemba 19 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichowashirikisha maofisa afya, wakuu wa vituo vya afya na zahanati, maofisa watendaji wa vijiji na kata wilayani humo amesema oparesheni ya kuwasaka watu hao ni lazima itekelezwe ndani ya siku saba.
Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge akisistiza jambo wakati akitoa maelekezo ya kusakwa watu wote wasiyo na vyoo katika kaya wilayani humo.Picha na Samwel MwangaAmesema kuwa oparesheni hii inalenga sio tu kukomesha ugonjwa wa kipindupindu, bali pia kuongeza ufahamu kwa wananchi juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira na afya ya jamii kwa ujumla.
Amesema kuwa watu hao watakaokamatwa na kupigwa faini y ash 50,000 kwa mujibu wa sheria ya ndogo ndogo za halmashauri za usafi wa mazingira katika halmashauri hiyo pia wanapaswa kujenga choo na kukitumia.
“Tuna sheria ndogondogo ndani ya halmashauri yetu,kaya isiyo na choo itatozwa faini ya Tsh 50,000 na pia tunawataka wajenge choo na kukitumia maana kuna wengine wana vyoo vinaitwa vya mabawana afya tu hawavitumi,”amesema.
Amesema ukosefu wa kwenye vyoo katika kaya hizo,unahatarisha maisha ya wakazi wa wilaya hiyo na ndiyo maana wilaya hiyo imekuwa ikukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu.
Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Maswa waliohudhuria kikao kazi cha mkuu wa wilaya hiyo,Aswege Kaminyoge(hayupo pichani) wa kuweka mikakati ya kupambana na kipindupindu.“Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri waandikie barua wenyeviti wote wa kamati za maendeleo za kata(wds)ambao ni madiwani ukiwajulisha juu ya operesheni hii na kesho serikali za vijiji wilaya nzima zikae na waelezwe jambo hili,kama ni elimu tulikwisha kutoa muda mrefu,”
“Nia aibu kwa wilaya yetu kwa kaya asilimia 38 ndizo zina vyoo na sisi tupo na tuko hapa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi, hivyo nendeni mkateleze haya tuliyokubaliana mkahakikishe kila kaya ina choo,”amesema.
Dk. Deogratius Mtaki aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa wilaya hiyo amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa ikifanya jitihada za kupambana na kipindupindu tangu kilipoingia katika wilaya hiyo kwa mara ya pili mwezi agosti 28 mwaka huu.
Dk Deogratius Mtaki aliyemwakilisha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa akieleza jinsi wilaya hiyo ilivyopambana na ugonjwa wa kipindupindu.Amesema hadi kufikia Desemba, 10, 2024 walikuwepo wagonjwa 58 na waliofariki ni watu wanne lakini hadi sasa hakuna mtu aliyelazwa kwa ugonjwa huu.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa,Onesmo Makota amesema kuwa katika jitihada za kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu, ni muhimu kuhakikisha kuwa viongozi na taasisi za serikali zinakuwa mfano bora kwa jamii kwa kuwa na vyoo.
“Kabla ya kuwachukulia hatua wananchi, ni muhimu kuhakikisha, taasisi zote za serikali, kama shule, vituo vya afya, na ofisi za umma, zina vyoo bora na vinavyofanya kazi ili kuonyesha mfano mzuri kwa wananchi,”amesema.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Kenan Kihongosi amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri katika mkoa huo kuhakikisha wanamaliza ugonjwa wa kipindupindu ndani ya kipindi cha siku saba kuanzia desema 18 hadi 24 mwaka huu ambacho kimedumu kwa mkoa huo kwa mwaka mmoja na miezi miwili.
Post a Comment