HEADER AD

HEADER AD

JAMII YATAKIWA KUTOIONA SANAA YA UIGIZAJI KAMA UHUNI

>> Vijana wa Nyakonga Tarime vijijini wazindua filamu iliyoigizwa kijijini

>>Bado kuna changamoto ya vijana wa kike wa kijijini kujiunga na sanaa

>> Nyambari Nyangwine, Simion Kilesi waunga juhudi za vijana wachanga fedha ununuzi wa vifaa

Na Dinna Maningo, Tarime

IMEELEZWA kuwa bado jamii ya watu waishio vijijini ina uelewa mdogo juu ya sanaa ya uigizaji huku kukiwa na mwamko mdogo wa vijana wa jinsi ya kike kujitokeza kujiunga na sanaa ya uigizaji licha ya kwmaba ni njia mojawapo ya kujipatia ajira .

Jamii ya watu waishio vijijini wametakiwa kuiona sanaa ya uigizaji kama ajira zingine na kwamba vijana wanapojitokeza kujiunga na kazi za sanaa ikiwemo ya uigizaji ,uimbaji wanapaswa kuwaunga mkono ili wayafikie malengo yao katika tasnia ya sanaa.

        Wananchi wa Kata ya Nyakonga wakiwa wameshiriki kwenye uzinduzi wa filamu ya Himaya ya Nyakonga Februari, 23, 2025

Akizungumza katika uzinduzi wa filamu ya vijana wa Kata ya Nyakonga iliyopewa jina la 'HIMAYA YA NYAKONGA' uliofanyika Kijiji cha Magoto, Februari, 23, 2025, Kada wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Magita aliyemwakilisha Mbunge mstaafu Jimbo la Tarime ,Nyambari Nyangwine katika uzinduzi wa filamu akiwa kama mgeni rasmi amewaomba wanajamii kuipenda sanaa na wasiwe na mitazamo hasi hususani kwa wasichana wanaojiunga na sanaa.

" Tusione sanaa ya uigizaji kama ni ya uhuni ni kazi kama kazi nyingine. Kazi ya sanaa ni kuelimisha, kuburudisha, kuonya na kukosoa. Tuwaruhusu vijana wetu wakiwemo wa kike wawekeze kwenye sanaa" amesema Daniel.

Amewataka wanakikundi kusajili kikundi chao ili kiweze kupata mikopo kwani serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitoa mikopo kwa vijana wakiwemo wasanii ili waweze kujiinua kiuchumi.

        Wananchi wa Kata ya Nyakonga wakiwa wameshiriki kwenye uzinduzi wa filamu ya Himaya ya Nyakonga Februari, 23, 2025

" Hiki kikundi kisajiliwe  bodi ya fimalu  na Basata ili mpate mikopo . Rais Samia anawajali wasanii hata majuzi tulimuona akishiriki kwenye tuzo za wachekeshaji.

" Lakini tunaona familia ya marehemu mzee Majuto ilizawadiwa milioni 30 kwa mchango wake wa kuchekesha, hafla iliyokuwa imeandaliwa na msanii Omy Dimpozi" amesema Daniel.

Daniel amesema kuwa katika kuunga juhudi za wasanii Nyambari Nyangwine amechangia Tsh. Milioni 2 ambapo awali alitoa Tsh. Milioni 1.4 kwa ajili ya maandalizi  ya uzinduzi na kwamba Nyambari ataendelea kuunga juhudi za wasanii hao wa uigizaji.

       Danieli Magita akiwasilisha fedha zilizotolewa na Nyambari  Nyangwine wakati wa uzinduzi wa filamu ya Himaya ya Nyakonga , akiwa amesimama na Kada wa CCM 

" Nyambari Nyangwine amesema kuwa ataendelea kuwachangia kadri mtakavyohitaji msaada, na hata sasa amewaleta waandishi wa habari hapa ili kuripoti tukio lenu watu wawaone wajue kumbe hata vijijini kuna watu wana vipaji.

" Nyambari Nyangwine hana mambo ya koo yeye ni Mwirege lakini amesaidia vijana wa koo ya Nyabasi , yeye anaangalia uwezo wa mtu katika kupambana katika maendeleo" amesema Daniel.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyakonga, Simion Kilesi nae hakuwa nyuma, alichangia Tsh. Milioni 1.1 huku wananchi nao wakimuunga fedha ambapo jumla ya kiasi cha Tsh. Milioni 3.7 zilichangwa.

       Mwigizaji wa filamu ya Himaya ya Nyakonga Doricas Johannes akimlisha keki Diwani wa Kata ya Nyakonga Simion Kiles

Hitaji ni pesa Tsh. Milioni 4.7 na hivyo kubaki zikihitajika Milioni 1 kukamilisha hitaji la fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kurekodia kazi ya sanaa katika uigizaji.

"Nimefurahi sana waalikwa mmeweza kufika kuwaunga mkono vijana wetu . Tukio hili ni geni ndani ya Kata ya Nyakonga na halmashauri ya wilaya ya Tarime .

" Nawapongeza vijana kwa kunishirikisha , tunamshukuru Nyambari kutusaidia maendeleo alitupatia vitabu na sasa amechangia vijana , na mimi nawaunga kwa Tsh. Milioni 1.1 naomba na wananchi mniunge" amesema Diwani Simon.

Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) kata ya Nyakonga, William Daudi Nyamali
amewaomba vijana kusonga mbele  " Hiki kinachofanyika hapa kinatokana na umoja wa vijana , haya ni matunda ya jumuiya ya vijana . Kuna wakati walikata tamaa lakini niliwashauri tusonge mbele na leo wamezindua filamu" amesema.

        Katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) kata ya Nyakonga,    William Daudi Nyamali akizungumza 
 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakonga Makomo Magabe amewapongeza vijana kwa kujihusisha na sanaa ambao ni wa kwanza kuibuka katika Kijiji chake huku akiwahimiza kuchapa kazi ili wajekuwa wasanii wakubwa.

          Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakonga Makomo Magabe 

Mwenyekiti wa kikundi cha Nyakonga Film Group Chacha Isaya amewapongeza watu waliojitokeza kuwashika mkono akiwemo Nyambari na Diwani wa kata hiyo na kuahidi kuwa ndoto zao ni kufahamika kimataifa .

"Tunamshukuru sana Nyambari kwa kusikia ombi letu, tulipompigia simu hakusita alituchangia fedha. Mimi mwenyewe simjui kwa sura ,tulipata namba ya simu tukampigia nae hakusita akatuchangia .

      Mwenyekiti wa kikundi cha Nyakonga Film Group Chacha Isaya akitoa shukrani

" Tunamshukuru sana tunaomba asituchoke, pia tunamshukuru Diwani wetu , viongozi wa CCM ,serikali ya Kijiji cha Nyakonga kwa kutuunga mkono hadi kufanikisha zoezi hili. Tumezindua filamu ukitaka kuipata ingia tu YouTube andika Himaya ya Nyakonga utaweza kuona tulichoigiza.

" Lengo letu ni kufika mbali, tuna mipango tuje kuwa wasanii wakubwa ambao kazi zao zinafanyiwa huku huku kijijin, tunataka watu wajue kwamba usanii sio mpaka ukaishi Dar kwamba ukiishiwa huko ndio utatoboa" amesema Marwa.

Akieleza changamoto amesema mwamko bado ni mdogo kwakuwa ni meneo ya vijijini " Kijijini hawakubali kazi ya sanaa wakati sanaa ni kazi kama kazi nyingine . Pia vijana wa kike ni wachache wapi 7 ambapo wakitume ni 23.

       Mbunge mstaafu Jimbo la Tarime Nyambari Nyangwine na mmiliki wa kampuni ya Nyambari Nyangwine Foundation 

" Tulianza na wasanii 4 tukaendelea japo tulikatishwa tamaa  , wapo walioacha lakini wengine tumevumia na sasa tupo watu 30 kati ya hao wasichana ni 7 tu".

Katika uzinduzi huo wameshiriki viongozi mbalimbali wakiwemo wa chama hicho ngazi ya Matawi na kata, baadhi ya viongozi wa serikali ngazi ya  vitongoji,vijiji na na kata, OCS kituo cha Borega, wameonesha kufurahishwa kwa namna vijana ambavyo wameamua kujitafutia fedha kupitia sanaa ya maigizo na kuwaombea mafanikio.

Mwigizaji wa muda mrefu aishiye Dar es Salaam Isaya Ryoba , ambaye ameigiza kwenye filamu ya Himaya ya Nyakonga, amesema maudhui yaliyobebwa kwenye filamu hiyo yamejikita katika kuelimisha jamii masuala mbalimbali ya kijamii na kupinga Mila potofu.

     Mwigizaji wa muda mrefu anayeishi mkoa wa Dar es Salaam Isaya Ryoba akizungumza 















No comments