HEADER AD

HEADER AD

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUTOA ELIMU YA SHERIA PWANI

Na Gustaphu Haule, Pwani

KAMPENI ya msaada wa Kisheria inayofanyika chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan (Mama Samia)kupitia  Wizara ya Katiba na Sheria, inatarajia kuanza kutoa msaada wa kisheria kwa Wananchi wa mkoa wa Pwani 

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa taarifa hiyo Februari ,22 ,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kujitokeza katika kampeni hiyo ili waweze kutatuliwa changamoto zao.

        Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge,akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu kuhamasisha ananchi kujitokeza kushiriki katika kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Kunenge amesema kuwa kampeni hiyo itafanyika siku tisa kuanzia Februari 25, hadi Machi 5, 2025 lengo la kampeni hiyo ni kutatua migogoro mbalimbali hususani ya ardhi ambapo jopo la wanasheria watashiriki kutoa huduma hiyo kwa wananchi katika wilaya zote za mkoa huo.

Kunenge amesema kuwa katika kampeni hiyo ambayo tayari imekwisha tolewa katika mikoa 19 ya Tanzania Bara imelenga kutatua changamoto za kisheria kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kugharamia huduma hiyo.

"Wananchi wapo wengi ikilinganishwa na wanasheria hivyo kwa kuona hilo Rais wetu mpendwa ameona ni vema wananchi wakapata huduma hii bure ili changamogo zao ziweze kutatuliwa kwa wakati na kwa haki"amesema Kunenge 

Kunenge amesema kuwa kampeni hiyo itaanza Februari 25 na kumalizika Machi 05, mwaka huu na kwamba wanasheria hao watawasaidia wananchi kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria.

      Msaada wa Kisheria wa Mama Samia

Mbali na hilo Kunenge amewataka wananchi wenye changamoto za kisheria ikiwemo migogoro ya ardhi na  ndoa kushiriki kikamilifu ili kupewa msaada huo ambao utatolewa bure bila malipo yotote.

"Gharama zote zimelipwa na serikali hivyo kilichobaki ni muitikio wa wananchi kushiriki kupata huduma, niwatake  wajitokeze kwa wingi ili changamoto zao zitatuliwe na malengo ya serikali yaweze kufikiwa"amesema Kunenge.


No comments