HEADER AD

HEADER AD

TAWIRI KUONDOA KERO YA MAMBA KIJIJI CHA KWAISEWA

Na Mwandishi Wetu, Korogwe

TAASISI ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii iko uwandani kwa wiki moja sasa wakiwa wamepiga kambi kijiji cha Kwaisewa eneo lililo na changamoto kubwa ya Mamba wanaohatarisha maisha ya wananchi.

Timu hiyo ikiongozwa na Dkt. Janemary Ntalwila ambaye ni mkuu wa kitengo cha habari na Elimu na mtaalamu wa kudhibiti migongano baina ya wanyamapori na watu akiwa na msaidizi wake Revocatus Meney Mtafiti na mtaalamu wa kudhibiti migongano baina ya  wanyamapori na watu.

Wataalam hao wameendelea kushirikiana na viongozi wa wilaya na Kijiji cha Kwaisewa katika upimaji na uhakiki wa eneo la ujenzi wa Kizimba katika mto Pangani kijijini hapo.

Akizungumza na Viongozi wa Kijiji na wananchi wanaoathirika,
Dkt. Janemary amewataka wanakijiji cha Kwaisewa kutoa ushirikiano na kuzingatia maelekezo ya matumizi ya Kizimba kitakapokamilika ili kupunguza athari tajwa. 

Revocatus Meney akiongoza mafundi wabobezi katika kazi hii ya ujenzi wa Vizimba, ametoa rai kwa wananchi kushiriki kwa dhati ili kukamilisha ndani ya muda mfupi.

"Kwa sasa ujenzi huko hatua ya pili ya upimaji wa eneo hatarishi na uwekaji alama sehemu Kizimba kitakapojengwa. Kazi inaendelea na maandalizi ya vifaa vyote yamekamilika " amesema .






No comments