HEADER AD

HEADER AD

MASAIBU MANNE ANAYOPITIA KIZZA

KIONGOZI wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye Yuko jela kwa zaidi ya miezi mitatu sasa.

Amewekwa kwenye chumba kidogo, katika jela ya Luzira, moja ya jela zenye ulinzi mkali zaidi Uganda.

Kwa mujibu wa mkewe, Winnie Byanyima chumba hicho chenye giza, ni kama uchochoro, na ni maalumu kwa ajili ya watuhumiwa wa ugaidi. Na kumfikia inakubidi kupitia karibu milango saba iliyofungwa na makufuli.

"Nilimtembelea Kizza Besigye kwenye selo yake, alikuwa amelala kwenye kitanda chumba kidogo ambacho kimechukua chumba kizima. Kulikuwa na milango sita au saba niliyopita mpaka kumfikia', alisema Winnie akinukuliwa na vyombo vya habari vya Uganda siku chache zilizopita.

Yuko hapo kwa muda sasa, baada ya kukamatwa kwa utata huko Nairobi Kenya, Novemba 16, 2024, alipokwenda kwa shughuli zake. Akasafirishwa usiku wa manane kupelekwa Uganda, kabla ya kufunguliwa mashitaka ya kumiliki silaha kwenye Mahakama ya kijeshi, siku mbili baadaye.

Hata hivyo kesi yake imehamishiwa katika Mahakama ya kiraia na Ijumaa iliyopita (Februari 21), alionekana kwa mara ya kwanza kwenye Mahakama hiyo akiwa kwenye kiti cha magurumu matatu akiendelea kuonekana dhaifu kiafya.

Lakini katika mahakama ya kiraia Dkt. Besigye alifunguliwa mashataka mapya ya uhaini, na hivyo kuashiria kesi za awali alizokuwa akikabiliwa nazo katika mahakama ya kijeshi zimekufa. Uamuzi wa Mahakama ya juu nchini humo uliotolewa Januari 31, kisheria uliikata makali mahakama ya kijeshi. Hata hivyo ataendelea kushikiliwa mpaka Machi 7, 2025 kesi yake mpya itakapotajwa tena katika Mahakama ya kiraia.

Kwa hisia za mkewe, Besigye anashikiliwa kwenye mazingira duni akisema kuwa. Lawama nyingi kuhusu yanayomsibu Besigye, yanaelekezwa kwa Rais Yoweri Museveni na serikali yake, ambapo mara kadhaa imekuwa ikikanusha kumpitisha kwenye masaibu. Hata muonekano wake wa sasa, akiwa chini ya mamlaka za jela nchini humo, lawama ni kwa Serikali.

''Katika hili, Dk Besigye, alikuwa kwenye mgomo wa kutokula. Hiyo ni sehemu ya sababu ya yeye kuwa dhaifu kunakoonekana kwenye picha zilizoko magazeti. Je! huo sio ulaghai usio na msingi? alisema Rais Museveni Jumanne iliyopita, akizungumza hali ya kiafya na kukamatwa kwa Besigye.

Yanayopitia sasa ni machache na ni sehemu tu ya masaibu mengi aliyowahi kupitia mwanasiasa huyu, aliyewahi kuwa daktari binafsi wa rais Museveni na mwanajeshi mstaafu. Na masaibu haya alianza kuyaonja hasa kuanzia mwaka 1999, baada ya kuchapisha andiko 'kali' lilikosoa Serikali na chama cha Museven cha NRM lililoitwa: "An Insider's View of How the NRM Lost the Broad Base". Andiko linalochambua jinsi NRM ilivyopoteza ushawishi wake na kuachwa na wafuasi wake wa awali. Na juhudi zake za kuwania urais mara nne na mara zote kushindwa dhidi ya rais Museveni aliyetawala taifa hiyo kwa miongo karibu minne, zinazidi kumpitisha pagumu.

1. Kukamatwa na kusekwa jela mara kwa mara

Kizza

Chanzo cha 

Maelezo ya picha,Kizza katika moja ya purukushani za kukamatwa na Polisi

Besigye sasa ana miezi mitatu yuko jela, sio mara ya kwanza wala sio mara moja kutupwa jela kwa tuhuma mbalimbali. Amekuwa akikabiliwa na kutupwa jela mara kwa mara, jela ni sehemu ya maisha yake. 

Kamata kamata ya Besigye ilianza kuonekana hasa baada ya kuwania urais kwa mara ya kwanza mwaka 2001. Baada ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Museveni, alikamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Serikali ikieleza alikuwa nyuma ya kundi la waasi la People's Redemption Army (PRA), lililokuwa katika nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia Kongo (DRC). Alipotangaza nia ya kuutaka urais kwa mara ya pili akakamatwa tena, ilikuwa Novemba 2005, ikiwa ni miezi michache kabla ya uchaguzi wa 2006.

Safari hii akidaiwa kuwa mhaini na mbakaji, tuhuma alizozikana. Kukamatwa kwake kulileta hasira nyingi Uganda, wengi wakiamini, ni hila ya walio madarakani kutaka asigombee urais. Akapewa dhamana na Mahakama ya juu nchini kabla ya muda mfupi kukamatwa tena na kurejeshwa jela safari hii kwa tuhuma za ugaidi na kumiliki silaha kinyume che sheria

Kuanzia hapa ikawa ni mfululizo wa kukamatwa na kuswekwa ndani mpaka kukamatwa kwake hivi karibuni jijini Nairobi na kutupwa ndani, anakosota mpaka leo kwa tuhuma za ukutwa na silaha.

2. Kupigwa, kudhalilishwa na kuwekwa vizuizini

kizza

Chanzo cha picha,

Maelezo ya picha,Kizza Besigye akiwa amekaa chini kwenye Kituo cha Polisi cha Kasangati baada ya kushikiliwa na kukumbana na mabomu ya machozi ya polisi mapema katika maeneo ya Mulago, Kampala. Hii ilikuwa ni mara ya nne kukamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja mwaka 2011.

Ukiacha kukamatwa na kupelekwa jela, si mara moja Besigye amewekwa kizuizini kwa sababu kadha wa kadhaa. Alishawekwa kizuizini Nile Hotel kwa miezi miwili mwaka 1981, akituhumiwa kushirikiana na waasi dhidi ya Serikali ya Rais Milton Obote.

Ukamatwaji wake wakati mwingine unakohusishwa na vitendo vya kupigwa na kudhalilishwa, wengi huukosoa wakihusishwa na ukiukaji wa haki za binadamu. Kuanzia madaktari wenzake wa zamani Nairobi, wanaharakati na wanasiasa wa ndani na nje ya nchi mpaka mashirika yanayotetea haki za binadamu.

Ripoti za Human Rights Watch (2021) na Amnesty International (2020) zilioonyesha kuwa kukamatwa na kutupwa jela kwa wapinzani wa kisiasa nchini Uganda ikiwemo Besigye, kumesababisha madhara ya muda mrefu kwa afya ya akili na mwili, ukiachilia mbali ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia. 

Baadhi ya milolongo ya matukio ya Kizza


Maelezo ya piKizza akiondoa moja ya vizuia kwenye moja ya makazi yake alivyowekewa na Polisi kuzuia kuingia ama kutoka kwa watu

• 1981 - Aliwekwa kizuizini Nile Hotel

• 1999: Alifunguliwa mashtaka kwa kuchapisha andiko lake la ukoasoaji Serikao lililoitwa "An Insider's View of How the NRM Lost the Broad Base" na kushtakia katika mahakama ya kijeshi

• August 2001: Alikimbilia uhamishoni Afrika Kusini, kulinda usalama

• Novemba 2005: Alikamatwa kwa tuhuma za uhaini na ubajaki

• April 2011 Alikamtwa kwa katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya vyakula

• Oktoba 2012: Alikamatwa kwa kuwahutubia wafanyabiashara

• 2016: Alikamatwa na jeshi wakati akijipashisha kama Rais wa wananchi, siku moja kabla ya Museveni kuapishwa

• Mei, 2022: Alikamatwa tena kwa kupinga kupanda kwa bei ya vyakula

• Novemba 2024: Alikamatwa Nairobi na kukutwa na silaha ingawa baade imebadilishwa na kuwa kesi ya uhaini.

3. Msururu wa kesi na kukimbia nchi

Kizza

Chanzo cha picha

Maelezo ya picha,Kesi za uhaini, ubakaji na kumiliki silaha kinyume cha sheria ni baadhi ya zinazomkabili marakwa mara Kizza

Besigye ni mganda, lakini mara kadhaa amesema, anahofia usalama wake nchini humo. Ukiukwaji wa haki zake unamfanya ajihisi salama akiwa nchi nyingine zaidi kuliko nchini kwake. Kwa sababu ya kamatakamata kutupwa jela na 'kubambikiwa kesi' kama mwenyewe anavyonukuliwa, amewahi kukimbia nchi mara kadhaa.

Kesi ya sasa ilipokuwa katika Mahakama ya kijeshi ilikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na silaha, ilipopelekwa kwenye mahakama ya kiraia akasomewa mashataka ya uhaini Ijumaa ya Februari 21, 2025. Mwaka Juni, 2001 alikamatwa kwa makosa kama hayo, kesi ambayo haikuendelea. Alikuwa na kesi nyingine ya uhaini na ubakaji mwaka 2005, alipokamatwa wakati wa kampeni za Uchaguzi.

Kesi za uhaini, uchochezi, ubakaji, kumiliki silaha ni baadhi ambazo amekuwa akituhumiwa nazo mara kadhaa. Zingine zimefika Mahakamani, zingine zimeishia njiani kabla ya kufikishwa mahakamani.

Mara baada ya heka heka ya kuwe kwa kizuizini Nile Hotel mwaka 1981, baadaye, mwaka 1982 alikimbilia Nairobi kabla ya kujiunga na Musevi kwa mapambano ya msituni.

Aliendelea kukimbia hapa na pale lakini matokeo ya uchaguzi wa 2001, zimwi la kuandamwa kwa Besigye kuliongozeka na kufuatiliwa na watu aliodai ni wa usalama na hivyo aliamua kukimbilia Afrika Kusini.

Aliishi huko kwa miaka minne. Kabla ya kurejea mwaka 2005, ambapo pamoja na mambo mengine kushiriki uchaguzi wa mwaka 2006 ambapo ilishindwa tena na Museveni.

Andiko lake la mwaka 1999 lililoituhumu NRM kuwa chama kinachoongozwa na dikteta mmoja, alifikishwa kwenye Mahakama ya kijeshi, "kwa kutoa maoni yake kwenye jukwaa lisilostahili". Hata hivyo baadae mashtaka yaliondolewa baada ya kuomba radhi.

4. Kukabiliwa na adhabu ya kifo?

Kizaa

za

Chanzo cha picha,

Maelezo ya picha,Besigye akiwasili jijini Nairobi, Kenya (April 29, 2011) kwa ajili ya matibabu, siku chache baada ya kutoka jela, alikoshikiliwa kwa wiki moja

Kesi yake tata inayomkabili sasa imehamishwa kutoka Mahakama ya kijeshi kwenda ya kiraia. Hii ni baada ya makelele mengi kupigwa bungeni, nje ya bunge na hata jumuia za kimataifa kuhoji ni kwanini ashitakiwe kwenye Mahakama ya kijeshi wakati yeye si mwanajeshi? alishastaafu miaka mingi. Machi 7 mwaka huu atarejeshwa tena Mahakamani.

Wakati akiendelea kupitia masaibu ya kuishi jela tangu Novemba mwaka jana, kwa mujibu wa sheria za Uganda, ukikutwa na hatia ya vitendo vya uhaini adhabu yake ni kifo. 

Hivyo kwa Besigye, wafuasi wake na wengine wanaomuunga mkono, kesi hii ina maana kubwa kwa upande wao. Kwa sababu kama atakutwa na hatia kwenye kesi ya sasa maana yake adhabu itakayomkabili Besigye ni hukumu ya adhabu ya kifo. 

Haya ni masaibu aliokutana nayo si mara moja, kutokana na aina za kesi zinazomkabili. Serikali na hata Rais Museveni mara kadhaa, amekana kuhusika na yanayompata Kizza. Hoja hapa, je atavuka kiunzi cha masaibu haya, akianza na kesi inayomkabili sasa yenye adhabu ya kifo?

Chanzo : BBC

No comments