HEADER AD

HEADER AD

MAWAZIRI SADC ,EAC WAKUTANA KUZUNGUMZIA MZOZO WA DRC


g

Chanzo cha picha,SADC

MAWAZIRI wa SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC wamekutana  jijini Dar es Salaam, Tanzania kujadili mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) kabla ya kikao cha Marais wa jumuiya hizo kitakachofanyika Jumamosi.

Lengo ni kutafuta suluhu ya mzozo mjini Goma, mashariki mwa DRC.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao wameuteka mji wa mashariki wa Goma, wamekuwa wakikabiliana vikali na majeshi ya serikali ya DRC.

Kulingana na Umoja wa Mataifa zaidi ya miili 2,000, ilipatikana imetapakaa mjini Goma wiki jana kufuatia makabiliano baina ya M23 na wanajeshi wa serikali.

Kongamano la viongozi wa SADC na EAC linafanyika huku kukiwa na changamoto ya kuwaleta wadau wote wa mzozo wa DRC.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi, akiapa kutozungumza na waasi wa M23, huku EAC ikipendekeza majadiliano kati ya wote wanaohusika kwenye mzozo huo.

''Suluhu mojawapo la mzozo huu ni kuwawaleta wanasiasa na wadau wote wa mzozo huu katika meza ya mazungumzo mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Maina Karobia katika mazungumzo na BBC.

''Natumai kwamba kongamano la Dar es salaam la jumuiya za SADC na Afrika Mashariki watavileta vikundi vyote kwenye meza ya mazungumzo, shida zao zitatuliwe vikubaliwe kuwa vitawekwa kwenye serikali na kunyang’anywa silaha’’, alipendekeza Bw Karobia.

No comments