HEADER AD

HEADER AD

MME AULIWA NA MKEWE AKISHIRIKIANA NA WATOTO WA KAMBO


>> Wananchi wateketeza mali

Na Alodia Dominick, Kyerwa

FRANCES Butoto (70) mkazi wa kijiji cha Kishanda kata ya Kibare wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameuawa ambapo tukio hilo litendwa na mke wake pamoja na watoto wa  kambo kisha mwili wake kuutumbukiza kwenye shimo la choo.

Chanzo cha mauaji kinadaiwa kinatokana na migogoro ya kugombania mali ambapo baada ya tukio hilo wananchi wameharibu mali mbalimbali za familia hiyo ikiwemo magari 2.

Tukio hilo limetokea Februari 16, 2025 na mwili wa marehemu ulikutwa umetqumbukizwa kwenye shimo la choo ambacho kilichimbwa shambani muda mrefu wakati wananchi wakiendelea kumtafuta marehemu waligundua choo ikiwa imefunikwa udongo mpya na kuanza kuifukua hivyo kubahatika kuukuta mwili humo.

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Kagera Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa,  bado jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tukio hilo na linakamilisha taarifa zake kuweza kubaini gharama ya mali zilizoharibiwa na wananchi pamoja na namba za magari  yaliyoteketezwa kwa moto.

          Baadhi ya mali zilizoharibiwa na wananchi baada ya Frances Butoto kuuawa na mke wake na watoto wa kambo wakihitaji mali za urithi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kishanda kata ya Kibale Nshekanabo Thomas amesema kuwa, mama huyo alikuwa na watoto wake ambao alihitaji warithi mali za marehemu wakati walikuwa wamezaliwa kwenye familia nyingine tofauti na alipoolewa mama yao jambo ambalo lilisababisha mgogoro wa mara kwa mara na marehemu huyo.

Amesema katika maisha ya marehemu Frances Butoto alikuwa na mgogoro na mke wake Frola Bitakanile na alikuwa ameishasuruhishwa mara kadhaa na mwenyekiti wa kitongoji cha Kishanda B.

"Mama huyo alikuwa na watoto  ambao alihitaji warithi mali za marehemu wakati walikuwa wamezaliwa kwenye familia nyingine tofauti na aliyoolewa mama yao" .

Thomas amesema tukio la mauaji ya Frances lilibainika baada ya kijana wake mkubwa Renatus Frances kwenda nyumbani kumuona baba yake bila mafanikio na alipomuuliza mama yake wa kambo aliambiwa ameondoka nyumbani siku nne zilizopita na huyo hajui alipo.


" Kijana huyo alionyesha kuwa na wasiwasi na alipopiga simu ya baba yake ilikuwa haipatikani, hivyo ilimulazimu kwenda kwa mwenyekiti wa kitongoji kutoa taarifa ya baba yake kutoonekana kwenye mazingira.

" Mwenyekiti wa kitongoji alimuita mke wa marehemu na kumhoji mwanamke alimwambia hajui alipo ndipo mwenyekiti wa kitongoji alimpigia mwenyekiti wa kijiji ili amshauri ndipo alimshauri  kwanza watafute kwa ndugu, jamaa na marafiki zao labda anaweza kuwa alienda huko, walianza jitihada za kumtafuta bila mafanikio"Amesema.

Ameongeza " Baada ya kuona hayuko huko tulishauriana tukapiga ngoma wananchi wakakusanyika  wakaanza kumtafutia kwenye mashamba yake, katika shamba lake kulikuwa na shimo la choo limechimbwa muda mrefu na lilionekana juu kuna udongo mpya hivyo likatiliwa shaka wananchi wakaanza kulifukua” amesema Thomas.


Wakati wakiendelea kulifukua wameona box na hatimaye wakaona mwili wa mtu na wakagundua kuwa alikuwa ni yeye wanayemtafuta, ndipo waliwakamata mke wa marehemu na watoto wake watatu.

Amesema baada ya kupata mwili huo Februari 22, mwaka huu wamepiga simu polisi nao walifika wakiwa na mganga na kutoa mwili kwenye shimo kisha kuufanyia vipimo na baadaye waliruhusu mwili uzikwe.

Aidha baada ya marehemu kuzikwa wananchi walianza kuharibu mali kwa kukata mashamba ya migomba na kahawa, kubomoa nyumba, na kuchoma magari mawili kubwa la mizigo na gari dogo.
 
Mtoto wa Marehemu Renatus Francis Butoto alitaja chanzo cha kuuawa baba yake kuwa ni baada ya mama wa kambo na watoto wake kutaka kupewa mali ikiwemo mashamba na ugonvi huo ulikuwa umedumu kwa muda mrefu wakitaka kupewa mirathi katika eneo lisilo lao.

Nao baadhi ya wananchi wamesema wamechukizwa na kitendo hicho kilichofanyika kwa kuondoa uhai wa binadamu na kusema kata ya kibare imekuwa na matukio ya kuuzunisha ,na kuiomba serikali kuhakikisha inachua hatua kali kwa wanaofanya vitendo vya kiukatili kama hivyo.

Ikumbukwe kuwa mke wa marehemu ambaye ni Frola Bitakalanile aliolewa na mzee Frances akiwa na watoto wengine wakubwa na mzee huyo alikuwa tayari ameishakuwa na watoto wakubwa ambao mama yao alifariki na hivyo kumuoa Frola.



No comments