HEADER AD

HEADER AD

MZOZO WA DRC WAASI WAZIACHA HOI FAMILIA ZA WACONGO

Mzozo wa DRC: Waasi waziacha hoi familia za Wacongo, vita vikipamba moto

ghbn

Chanzo cha picha,Göktay Koraltan / BBC

Heshima anajikunja kwa maumivu anapojaribu kubadilisha upande wa kulala, jasho linamtoka. Ni mtoto mwenye umri wa miaka 13, amelala kwenye kitanda kwenye hema katika uwanja wa hospitali uliojaa watu katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Mguu wa kushoto wa Heshima umefungwa bendeji, tumbo lake lina alama za kuungua, na wazazi wake wote wawili wameuawa.

Jamaa yake, aitwaye Tantine, anatuambia ni nani wa kulaumiwa; waasi wa M23 - wakiungwa mkono na Rwanda ambao wanapambana na jeshi la Congo, linalojulikana kama FARDC. Waasi hao sasa wanadhibiti miji miwili mikubwa katika eneo hili lenye utajiri mkubwa wa madini, ambalo linapakana na Rwanda.

"Ilikuwa Jumapili," anasema. "Kulikuwa na mapigano kati ya waasi na FARDC. (Waasi) walirusha bomu, na nikapoteza watu sita wa familia yangu."

Uasi wa M23

j

Chanzo cha picha,Göktay Koraltan / BBC

Maelezo ya picha,Mwandishi wa habari wa ndani anasema vyombo vya habari huko Goma vinajizuia katika hali ya kutokuwa na uhakika

M23 wanajitangaza kama wapigania uhuru, wanaoleta amani na utulivu katika nchi iliyovurugika, na kiongozi aliyeshindwa Rais wa Congo, FĂ©lix Tshisekedi.

Ni kundi la waasi, linalojumuisha watu wa kabila la Watutsi, na limekuwa likisonga mbele tangu mapema mwaka 2022, likiteka maeneo mengi - kwa msaada wa wanajeshi 4,000 wa Rwanda.

Hayo ni kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaosema Rwanda ina "udhibiti wa mkubwa" juu ya kundi hilo - lakini Kigali na Rais wa Rwanda Paul Kagame wanakanusha.

Madhara ya kusonga mbele M23 yanaonekana katika Hospitali ya Ndosho, ambako Heshima inatibiwa.

Madaktari wanatatizika kuondoa mrundikano wa raia na wanajeshi waliojeruhiwa mwishoni mwa Januari, waasi walipouchukua mji wa Goma. M23 wanasema "waliukomboa" mji huo.

Idadi ya waliofariki katika mapigano hayo inakaribia watu 3,000, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Vyumba vinne vya upasuaji vinatumika kwa wakati mmoja - mchana na wakati mwingine usiku.

"Hali imekuwa mbaya kwa madaktari," anasema Myriam Favier wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC), ambayo inasaidia hospitali hiyo.

Madaktari hao wamekuwa wakilala katika vyumba vya upasuaji, anasema.

"Vifaa vyetu vya matibabu viliporwa mwanzoni kabisa mwa vita. Na tulikuwa na mmiminiko wa watu ambao haukutokea hapo awali - kati ya wagonjwa 100 na 150 kwa siku kwa wiki kadhaa."

Kwa sasa ni chini ya watu 10 kwa siku, kulingana na Bi Favier na sasa watu wanajaribu kurudi katika maisha yao.

Hali katika mji wa Goma

ij

Chanzo cha picha,Göktay Koraltan / BBC

Maelezo ya picha,Takriban watu 3,000 wanakadiriwa kuuawa wakati wa vita vya Goma

Unapotembea katika mji wa Goma, mitaa inavuma kwa pikipiki. Maduka mengi yamefunguliwa, na wauzaji katika magenge wamerudi na marundo yao ya vitunguu, parachichi na nyanya.

Wapiganaji wa M23 wenye silaha hawaonekani. Hawapo kwenye kona za barabara. Hawana haja ya kufanya hivyo. Kila mtu anajua wao ndio wanadhibiti mji.

"Watu wangemkubali shetani hapa, ikiwa wanaamini ataleta amani," anasema mwanaume mmoja.

Wengine wako makini sana. Mwandishi wa habari anasema, vyombo vingi vya habari "vinajidhibiti" juu ya kile wanachoripoti, wakisubiri kutathmini jinsi watawala wapya watakavyokuwa.

Mwanaharakati mmoja amenambia, wengi wa wanaharakati "wanaishi katika ukimya mkubwa" kwa sababu ya kuogopa kulipiziwa kisasi na waasi.

"Hiki ni kipindi cha wasiwasi zaidi katika historia ya Goma," anasema. "Naogopa, siku zijazo hazina uhakika."

Taarifa zinazokinzana za M23

Göktay Koraltan / BBC
Maelezo ya picha,Watu wameanza kubomoa mahema katika kambi ya Bulengo - moja ya kambi ya Goma kwa wale ambao wamekimbia makazi yao katika miaka ya hivi karibuni.

"Tarajia amani, usalama, maendeleo, upatikanaji wa ajira na siku zijazo zisizo na wakimbizi, rushwa wala njaa," anasema Willy Manzi, makamu gavana mpya wa M23 ambaye amerejea hivi karibuni kutoka Canada, alichapisha taarifa hiyo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Lakini maelfu ya watu ambao wametafuta hifadhi kutokana na mapigano katika miaka ya hivi karibuni katika kambi za Goma, wamepewa ujumbe tofauti.

Walipewa masaa 72 kuondoka. M23 wanataka kambi hizo zifutiliwe mbali, pamoja na makundi yoyote hasimu yenye silaha yanayojificha kwenye kambi hizo.

"Walikuja na kutuambia, 'Mna siku tatu za kuondoka," anasema Divine, 19, ambaye ana mtoto amempakata, na mwingine miguuni mwake.

"Tuliogopa kwa sababu hatuna pa kwenda. Nyumba zetu zimeharibiwa. Njaa inatuua hapa, lakini tutakwendaje nyumbani ambako hakuna chochote?"

Wakati akizungumza umati unakusanyika karibu yetu. Kuna miitikio ya kimya na nyuso zenye wasiwasi.

"Walikuwa maadui zetu na sasa ni majirani zetu," anasema mtu mmoja ambaye anaomba jina lake lisitajwe.

Nyumbani kwa Mungu ni kambi ya Bulengo - eneo la mahema meupe chakavu, yaliyowekwa kwenye miamba ya volkeno, kambi iliyozungukwa na vilima vya kijani kibichi.

Tulipowatembelea wengi walikuwa tayari wanafungasha mizigo, wakibeba vipande vya mbao na plastiki, na kukunja matandiko.

Baada ya kuwaamuru watu kuondoka katika kambi, M23 baadaye walisema "wanawahimiza kuondoka kwa hiari."

Lakini haionekani kuwa ni hiari kwa wengi wa waliohamishwa.M

Mgogoro wa Congo

hg

Chanzo cha picha,Göktay Koraltan / BBC

Maelezo ya picha,Familia zinahisi hazina chaguo ila kuondoka kambini - na itabidi wafunge safari ya kurudi nyumbani kwa miguu

Mashirika ya haki za binadamu yanasema ni mtindo wa unyanyasaji unaofanywa na waasi - ambao wanatuhumiwa kwa kushambulia raia kwa makombora, ubakaji na mauaji ya kiholela.

Shutuma kama hizo pia zimetolewa dhidi ya jeshi la Congo na washirika wao.

Mgogoro huu ni wa miongo kadhaa una mizizi yake - kwa sehemu - katika mauaji ya halaiki ya Rwanda ya 1994, karibu watu 800,000, wengi wao wakiwa Watusi, waliuawa na Wahutu wenye msimamo mkali.

Baadaye Wahutu wengi walikimbilia DR Congo, baadhi wakiwa ni wale waliohusika na mauaji ya halaiki. Rwanda inasema bado watu hao ni tishio.

Wakosoaji wanasema Kigali inatazama utajiri mkubwa wa madini wa DR Congo, ambao ni muhimu kwa teknolojia nyingi duniani ikiwa ni pamoja na kompyuta na simu za mkononi.

Kuna hofu inayoongezeka kwamba mzozo wa kudhibiti utajiri huu unaweza kusababisha vita vipya vya kikanda, na athari mbaya kwa Afrika.

Vyovyote vile - ikiwa historia ni mwongozo - hazina zilizo chini ya udongo, hazionekani kuwafaidisha watu hapa.

Turudi kwenye kambi ya Bulengo, ambako tulikutana na Alphonsine, aliyekuwa akiondoka na familia yake kubwa, akiwa ameinama na mzigo mzito mgongoni mwake.

Anasema yatakuwa ni matembezi ya siku mbili kufika katika mji wake, na hakukuwa na kitu kilichobaki. Nyumba yake ilisha haribiwa.

"Utaishije?" nilimuuliza.

"Nilitoka kwenye mateso," anasema, "na ninaondoka kwa mateso."

Chanzo : BBC 

No comments