HEADER AD

HEADER AD

WANAFUNZI SHULE YA MSINGI, MAPINDUZI, AZIMIO, SABASABA WASOMA WAKIWA WAMESIMAMA

>>Ni baada ya agizo la DC Tarime kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule.

>>Mwenyekiti wa Mtaa wa Sabasaba awaomba wadau msaada wa madawati

Na Helena Magabe Tarime

MWENYEKITI wa mtaa wa sabasaba  ambaye pia ni mlezi wa shule tatu zilipo mtaani kwake Sabato Marwa ameiomba halmashauri, wadau mbalimbali pamoja na Serikali kujitokeza kutoa msaada wa madawati.

Mwenyekiti huyo wa mtaa ameiambia DIMA Online, kwamba, zaidi ya wanafunzi 100 katika shule ya msingi Azimio, Sabasaba pamoja Mapinduzi zilizopo katika mtaa huo wanasoma wakiwa wamesimama na wengine kukaa chini sakafuni.

        Mwenyekiti wa mtaa wa Sabasaba,mjini Tarime Sabato Marwa akizungumza 

Sabato amesema baada ya DC Edward kutoa wito wazazi kuwapeleka watoto shule mwitikio umekuwa mkubwa hali ambayo imesababisha kuwepo uhaba wa madawati. 

"Hadi kufikia leo wanafunzi walikuwa hawajaingizwa kwenye mfumo maana ni wengi watoto zaidi ya 100. Nimewasiliana na walimu maana mimi ni mlezi wa shule hizo zote tatu, nilienda nikakagua wanafunzi wanasoma wamesimama wengine wamekaa chini.

" Baada ya DC kuhamasisha watoto waende shule hata kama hawajakamilisha mahitaji ya shule mwitikio umekuwa mkubwa mpaka walimu wanajiuliza wametokea wapi !. Shule iyojaa sana ni Mapinduzi. Naiomba serikali na wadau wa maendeleo watusaidie kutatua changamoto ya uhaba wa madawati"  amesema Sabato.

Amewashukuru wadau mbalimbali wanaomshika mkono katika kuchangia maendeleo ya shule " Hivi karibuni Mbunge wa viti maalumu Esther Matiko alichangia Tsh. 500,000 kwaajili ya kukarabati majengo ya shule ya msingi azimio.

" Mbunge wa Tarime mjini Michael Kembaki ameahidi kusapoti shule, kikundi cha Tarime nguvu moja kimemahidi vyombo 10 vya kuhifadhia uchafu,(dustbin) vile vile Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mara ameahidi kuchangia vifaa vya usafi katika shule zote tatu.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa ,hivi karibuni kwa kushirikiana na mdau wa maendelo Deogratius Meck alifanikisha watoto 18 wanaoishi mazingira magumu kupata mahitaji ya shule na nguo za shule na hivyo kujiunga na masomo.

" Wanafunzi wameenda shule ingawa  hadi kufikia Februari 17, 2025 wakati nazungumza na waandishi wa habari  wanafunzi walikuwa hawajaingizwa kwenye mfumo kutokana na wingi kiasi cha walimu kupata wakati mgumu kuwasajili wanafunzi hao zoezi la usajili linaendelea.

Pia amemshukuru mdau wa maendeleo Said Kisyeri Chambili kwa kuchangia 300,000 peza za kufufua kisima kilichokufa miaka mingi ambacho kilikuwa kinahudumia mitaa minne kwenye kata ya Sabasaba pamoja na Mitaa ya kata za jirani.

Mkuu wa wilaya Tarime, Meja  Edward Gowele amesema anatambua uwepo wa uhaba wa madawati na si kwa shule ya msingi Mapinduzi peke yake ni kwa wilaya nzima na hata nchi nzima na kuongeza kuwa, Halmashauri imeshaanza mchakato wa upatikanaji wa madawati.

       Mkuu wa wilaya Tarime, Meja  Edward Gowele akizungumza 

Amewapongeza wenyeviti pamoja na watendaji kwa kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto shule ambapo amesema Serikali imejitahidi kujenga miundo mbinu bora, elimu bure na mengineyo  lakini haiwezi kukamilisha vyote kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa hata Roma haikujengwa mara moja.

Amesema kuwa changamoto haziwezi kuisha mpaka pale mtu anapokuwa amefariki hivyo amewaomba wadau mbali mbali kuchangia madawati bila kujali itikadi zao wakati huo serikali ikishughulikia tatizo hilo. Vile vile amemwomba mwenyekiti kufanya harambe ili wananchi wachangie.



No comments