WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUONGOZA SAMIA MARATHON KIBAHA VIJIJINI
Na Gustaphu Haule, Pwani
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kuongoza mbio za polepole "Samia Marathon "zitakazofanyika Mlandizi Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani Josian Kituka, amewaambia Waandishi wa habari Februari ,20 katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM )Mkoa wa Pwani zilizopo Kibaha Mjini kwamba mbio hizo zinafanyika Februari, 22, 2025.
Kituka amesema kuwa maandalizi ya mbio za Samia Marathon yamekamilika na kwamba malengo yake ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Pwani Josian Kituka akizungumza na Waandishi wa habari leo Februari 20 katika ofisi Chama zilizopo Mjini Kibaha kuhusu kufanyika kwa Samia Marathon.
Amesema kuwa wameamua kutumia jina la Samia kwa ajili ya kumpa heshima Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amefanya kazi kubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi alichokaa madarakani.
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo Jumuiya wa wazazi mkoa wa Pwani imeona ni vyema kuandaa marathon hiyo ilikusudi waongeze kasi ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu ili kuhakikisha Rais Samia anashinda kwa kishindo.
Amesema kuwa mbio hizo zitaanzia katika viwanja vya shule ya msingi Mtongani na kuelekea barabara ya Ruvu ikiwa ni umbali wa Kilomita tano, na wengine watakimbia km tatu na mbili ambapo Waziri mkuu ataongoza mbio hizo kwa umbali wa kilomita tano .
"Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani imeandaa mbio za Samia Marathon ambazo zinafanyika Kibaha Vijijini na tunatarajia kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi" amesema Kituka
Kituka amesema katika mbio hizo wanatarajia kuwa na washiriki 7000 kutoka ndani ya mkoa na hata nje ya mkoa huku akiwaomba Wananchi wajitokeze zaidi siku ya tukio hilo.
Amesema kwakuwa jambo hilo limeandaliwa na mkoa kutakuwa na washiriki kutoka wilaya zote za mkoa wa Pwani huku akiendelea kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki mbio hizo kwakuwa hakuna kiingilio.
Hata hivyo, Kituka amesema kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia Samia Marathon itapambwa na burudani mbalimbali wakiwemo wasanii wa Bongo Fleva,bendi za muziki ikiwemo Twanga na kupepeta pamoja na vikundi vingine vya sanaa.
Samia Marathon kufanyika Mlandizi Kibaha Vijijini Mkoani Pwani Februari 22 mwaka huu.
Post a Comment