HEADER AD

HEADER AD

HALMASHAURI YA KIBAHA YAKUSANYA BILIONI 1.4 MAPATO YA USHURU WA HUDUMA

>> Mwaka uliopita ilikusanya Milioni 420 

Na Gustaphu Haule, Pwani 

HALMASHAURI ya Mji Kibaha chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Rogers Shemwelekwa imefanikiwa kupandisha mapato yatokanayo na ushuru  wa huduma (Service Levy)kutoka Tsh.Milioni 420 mpaka kufikia Tsh.Bilioni 1.4.

Ongezeko la mapato hayo ni katika kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni kuanzia  Machi 2024 hadi Aprili 2025.

Taarifa ya ukusanyaji wa mapato hayo imetolewa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Shemwelekwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi leo Aprili 29,2025 kikilenga kubainisha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2020)2025.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Kibaha Shopping Mall licha ya kuhudhuriwa na Madiwani hao lakini pia kiliwashirikisha watumishi mbalimbali wakiwemo Watendaji Kata na walimu.

Wananchi na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Mji Kibaha waliojitokeza kuhudhuria Baraza la Madiwani Aprili 29,2025.

Akizungumza katika Kikao hicho mkurugenzi huyo amesema kuwa mapato ya ushuru wa huduma za jamii yameongezeka kutokana na kuweka mipango madhubuti ikiwa pamoja na kuunda timu maalum ya ufuatiliaji.

Dkt.Rogers amesema kuwa aliteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Machi 9,2024 kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Kibaha na alipofika alikuta ukusanyaji wa mapato  yanayotokana na ushuru wa huduma za jamii ( Service Levy) kiasi cha Tsh. Mlioni 420 lakini mpaka sasa mapato hayo yamepanda mpaka kufikia Tsh Bilioni 1.4.

Amesema mafanikio ya ukusanyaji huo ni kutokana na ushirikiano anaohupata kutoka katika timu yake na watendaji mbalimbali wa Halmashauri hiyo ,Mbunge na madiwani huku akiahidi kuendelea kufanyakazi kwa ushirikiano.

         Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa (Pichani)akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi Aprili 29,2025 katika Ukumbi wa Kibaha Shopping Mall.

",Kwa moyo wa dhati napenda kutumia nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuniteua kuwa mkurugenzi wa halmashauri hii na mimi naahidi kufanyakazi kikamilifu kwa ajili ya kuhakikisha Kibaha inapata maendeleo zaidi,"amesema Dkt.Shemwelekwa.

Shemwelekwa amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana Kibaha yanatokana na Rais Samia kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba yeye na timu yake wanahakikisha kila fedha inayokuja wanaisimamia vizuri ili kufika malengo ya mheshimiwa Rais Dkt.Samia.

Ameongeza kuwa , kwa sasa Kibaha ipo katika mpango wa kujenga soko kubwa la kisasa ambalo litatumia zaidi ya Tsh. Bilioni 17 na kwamba soko hilo litakuwa na miundombinu mizuri ya barabara na hivyo kufanya wafanyabiashara wawe katika mazingira mazuri.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Musa Ndomba , amesema kuwa kwa aina ya mkurugenzi aliyekuwepo ameonyesha Jinsi gani anakiu ya kuifanya Kibaha Mjini isongembele ambapo amemtaka mkurugenzi huyo kuendelea kuchapakazi na kutimiza malengo ya wanaKibaha.

      Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba akiongoza kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika Aprili 29,2025 Kibaha Shopping Mall.

Ndomba , amesema kuwa pamoja na ongezeko la mapato hayo lakini Kibaha mjini kazi kubwa imefanyika ndani ya miaka mitano ikiwa pamoja na ukamilishaji wa miradi mingi ya maendeleo.

Ndomba ametaja baadhi ya  miradi iliyotekelezwa kuwa ni ujenzi wa vituo vya afya viwili,Zahanati tisa, ukarabati wa kituo cha afya mkoani na vifaa tiba kutoka serikali kuu, halmashauri pamoja Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.

Amesema,miradi mingine ni pamoja ujenzi wa Shule 11 za Msingi, Shule za Sekondari tisa za Sekondari,Shule za mchepuo wa kiingereza mbili,huku upatikanaji wa Maji ni asilimia 93.

Nae Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka, amempongeza mkurugenzi huyo na watumishi wote wa Halmashauri ya Kibaha mjini kwa namna ambavyo wameshirikiana kusimamia miradi ya maendeleo.

Hatahivyo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka,ametumia kikao cha Baraza hilo kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amewezesha mambo mengi hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

       Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini Mwajuma Nyamka akizungumza katika kikao cha baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Kibaha lililofanyika Aprili 29,2025 likiwa mahususi kwa ajili ya kuweka baina mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano .

Amesema kuwa Rais Samia amekuwa akitoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo Kibaha mjini lakini pia bila ya usimamizi mzuri wa mkurugenzi na watendaji wake uenda fedha hizo zingepotea na miradi ingekwama.

"Naipongeza halmashauri ya Kibaha mjini kupitia mkurugenzi wake Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa usimamizi mzuri wa miradi lakini pia tumeona miradi mingine imetekelezwa kwa mapato ya ndani ,"amesema Nyamka 

Nyamka amemsifu mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka kwa namna ambavyo amekuwa akisukuma gurudumu la maendeleo Kibaha na mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa Rais,Mbunge na madiwani .

Hatahivyo,Nyamka ametaka miradi yote ya Kimkakati lazima izingatie maslahi mapana ya pande zote ikiwemo Halmashauri, serikali na CCM kwakuwa Chama hicho ndio msimamizi wa utekelezaji wa ilani.

      Wananchi na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya Mji Kibaha waliojitokeza kuhudhuria Baraza la Madiwani Aprili 29,2025.


No comments