HEADER AD

HEADER AD

MWENYEKITI MTAA WA SABASABA WILAYANI TARIME AJIVUNIA MAFANIKIO KATIKA UONGOZI WAKE

>> Aeleza mafanikio ndani ya miezi minne tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti 


Na Dinna Maningo, Tarime

KWA mtazamo wa kijamii uongozi ni uwezo wa mtu au kundi kuongoza wanajamii katika kujenga mshikamano, maendeleo na ustawi wa pamoja .

Kiongozi wa jamii uhakikisha hali, usawa, amani, na utatuzi wa migogoro kwa nia ya busara. Kiongozi bora anapaswa kuwa na sifa mbalimbali zinazomuwezesha kuongoza kwa ufanisi.

Baadhi ya sifa hizo ; kiongozi anapaswa kuwa na maono awe ana dira na malengo ya muda mrefu ambayo uongoza hatua zake na za wale anaowaongoza.

Awe mwadilifu na anayepaswa kuwa mwaminifu, mkweli, na mwenye kushikilia maadili mema, awe na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati unaofaa.

Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufanisi, kusikiliza na kuelewa mahitaji ya wengine, awe na uwezo wa kulea na kukuza wengine. Kiongozi mzuri huwezesha na kuendeleza uwezo wa wale anaowaongoza.

Kiongozi bora anapaswa kuwa jasiri katika kukabiliana na changamoto na kufanya maamuzi magumu. Kiongozi bora anawajibika kwa matendo na maamuzi yake, na huonesha mfano kwa wengine.

Kiongozi bora ujenga na kudumisha uaminifu kati ya kiongozi na wale anaowaongoza ni msingi wa uongozi bora.

Kiongozi anayetambua na kuthamini michango ya wengine hujenga mazingira chanya ya kazi. Pia ana uwezo wa kujifunza na kubadilika, kiongozi bora hujifunza kutokana na uzoefu na kubadilika kulingana na mahitaji ya mazingira.

Hata hivyo , Si kila mtu anaweza kuwa kiongozi mzuri, bali ni wale waliokabidhiwa kipawa hicho na Mungu.

Katika maandiko matakatifu ya Mungu 'Biblia' kitabu cha Warumi 12 mstari wa 6-8 kinasema ; Basi kwakuwa tuna karama tofauti sawasawa na neema tuliyopewa, ikiwa ni ya unabii , na itumike kwa kadiri ya imani.

Ikiwa ni huduma , utumike katika huduma hiyo,mwenye kufundisha,na afundushe , mwenye kuonya na aonye, mwenye kutoa na atoe kwa ukarimu, mwenye kusimamia na asimamie kwa bidii na mwenye kurehemu na afanye kwa furaha .

Sabato mwenyekiti mpambanaji

Sabato Marwa ni Mwenyekiti wa mtaa wa Sabasaba katika kata ya Sabasaba wilayani Tarime mkoa wa Mara,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) aliyechanguliwa na wananchi katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba, 2024.

         Mwenyekiti wa mtaa wa Sabasaba, Sabato Marwa.

Mwenyekiti huyo ameonekana kuwa na kasi katika kuwatumikia wananchi mtaani kwake katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo utatuzi wa migogoro ya ardhi na uhamasishaji wa maendeleo.

Sabato Marwa anaanza na shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa mtaa na kueleza mafanikio ndani ya miezi minne katika uongozi wake.

" Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kunipa uzima na afya tele lakini pia nawashukuru wananchi wa mtaa wa Sabasaba kwa kuniamini na kunichagua ili niwatumikie" anasema.

    Elimu ya ardhi

Anaeleza mafanikio katika masuala ya ardhi " Katika miezi minne ya uongozi wangu tangu nichaguliwe, kupitia uongozi wa mtaa wananchi wangu zaidi ya 25 ambao walikua hawajapimiwa viwanja na wengine kukosa hatimiliki waliweza kupata elimu toka ofisi ya ardhi bure " anasema Sabato.

     Vikundi

Anasema uongozi wa mtaa umeisha kutana na vionozi wa vikundi 10 katika mtaa wa Sabasaba. Viongozi hao kwaniaba ya wanachama wao waliweza kupata elimu ya ujasiliamali kutoka idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya Mji Tarime.

            Wanataka wakiwa kwenye mkutano 

" Pia katika suala la kilimo vikundi hivyo vimeweza kupata elimu ya kilimo kutoka kwa Dr. Mango. Lakini pia mtaa wetu ulipata nafasi ya kua mwenyeji wa kampeni ya kisheria kutoka kwa Mama Samia Legal AID, ambapo pia vikundi na wananchi wa Sabasaba walipata nafasi ya kujifunza umuhimu wa kutatua migogoro yao nje ya Mahakama.

       Elimu

Anasema Watoto 18 ambao walikua mitaani wameweza kupelekwa shuleni na kupokelewa. Waliweza kushonewa sare za shule, wakapewa masweta, madaftali na penseli kwa ufadhili wa mdau wa maendeleo Deo Meck.

" Zaidi ya wanafunzi 300 wa darasa la kwanza walipata madaftali mawili na Penseli moja kila mwanafunzi katika shule zilizopo mtaa wangu ambazo ni shule ya Mapinduzi, Sabasaba na Azimio misaada iliyotolewa na Deo Meck. 

Mwenyekiti wa mtaa wa Sabasaba (kushoto) akipokea msaada wa madaftari, masweta na penseli kwa ajili ya kuwapatia wanafunzi uliotolewa na mdau wa maendeleo Deo Meck.

"Pia mdau mwingine ambaye ni mbunge wa viti maalum Ester Matiko kupitia Taasisi yake ya Matiko Foundation ilitoa Tsh. 500,000 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa shule ya msingi Azimio. 

" Katika michezo nimepeleka mipira kwenye shule ya msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio. Kila shule ilipata mpira 1 wa miguu kwa msaada wa Matiko Foundation" anasema.

 Sabato anasema kwamba , ofisi ya mtaa iliweze kujumuika katika ziara ya mkuu wa Wilaya wa Tarime, Edward Gowele ambae alifika shule ya msingi Sabasaba, Mapinduzi na Azimio kusikiliza kero baada ya kupokea changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa majengo na uhaba wa madawati.

 Mkuu wa wilaya ya Tarime Edward Gowele ( aliyesimama wa pili kushoto) akizungumza na wanafunzi .

" Kupitia ziara hiyo tulijionea wenyewe uhaba wa eneo ambapo mkuu wa Wilaya, Mhandishi wa Halmashauri pamoja na Walimu. Hali hiyo ilitulazimu  kuiomba Serikali kua na mpango wa Kujenga Ghorofa katika shule hizo kutokana na wingi wa wanafunzi huku kukiwa na uhaba wa eneo lakini pia tuliomba uzio uwekwe katika eneo la shule.

" Kupitia mdau wa maendeleo kampuni ya Soya alitoa msaada wa madawati 5 shule ya msingi Sabasaba na tukayakabidhi" anasema Sabato.

        Afya

Mwenyekiti huyo anasema wameweza kufanikiwa kuhimiza usafi wa mazingira na kudhibiti uchafu kwa vitendo kutoka maeneo mengine na hivyo kuimarisha mazingira ya mtaa kua safi na salama.

" Tuliomba wafadhili kampuni ya Mara Onaline inayojihusisha na masuala ya habari ikatupatia vifaa vya usafi kwa shule zote 3 zilizopo mtaa wa Sabasaba. Tulikiomba kikundi cha Tarime nguvu moja vifaa vya 10 vya Kuhifadhia taka kikatupatia.

      Maji

Anasema ili kuondokana na tatizo la uhaba wa maji kuna mchakato wa kutoa maji kutoka kwenye tenki la maji lililopo mlimani, kufufua kisima cha mtaa kilichokaa miaka 4 licha ya kuhudumia wananchi zaidi ya mitaa minne ya Kata ya Sabasaba.

" Mchakato huo wa kufufua kisima cha maji utaendeshwa na mdau Said Chambiri, lakini pia bado tunategemea mpango wa muda mrefu kutoka Serikali kuu ambao ni kutoa maji Ziwa Victoria" anasema.

   Ulinzi na Usalama

Mwenyekiti Sabato anasema mtaa wa Sabasaba ulikua na matukio ya uhalifu yaliyohatarisha usalama na kwamba  baada ya kuwa kiongozi amesimama vyema suala la ulinzi na usalama na kuwezesha baadhi ya watu kufikishwa Mahakamani.

" Kati yao wapo waliohukumiwa kifungo jela, wengine wamepata elimu ya kuacha uhalifu iliyotolewa na uongozi wa mtaa. Kwa sasa usalama wa mtaa unaridhisha kwa asilimia 70 japo lengo la mtaa tunahitaji usalama uwepo asilimia 100.

" Malengo kama mtaa ni kuhimiza taasisi, wafanyabiashara kuweka walinzi imara katika maeneo yao ya biashara, hii itapunguza kwa asilimia kubwa wimbi la wizi, lakini mtaa kuendelea na doria kwa kushirikia na Jeshi la Polisi nyakati zote iwe usiku au mchana hata pale tupatapo taarifa kutoka kwa wananchi.

       Barabara

Mwenyekiti huyo wa mtaa wa Sabasaba anaishukuru Wakala wa barabara za vijijini na mjini (TARURA) wilaya ya Tarime kukangua barabara zote katika mtaa , japo kutokana na mvua wameshindwa kuweka moramu.

" Serikali imeweka rami kwenye barabara 3 zinazopita mtaa wa Sabasaba ambapo ndani ya kata nzima mtaa wa Sabasaba tumebahatika kupata mradi huo kutoka TAKITCK." anasema.

      Ukatili wa kijinsia

UongozI wa mtaa katika kuungana na Serikali ambayo inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan inayopambana na vitendo vya ukatili, imefanikiwa kumfikisha mahakamani mzazi  mmoja aliyekuwa anashiriki kimapenzi na mwanae mwenye umri wa miaka 8.

" Mzazi huyo alikuwa anashiriki kimapenzi na mtoto wake, kitendo kilichopelekea mtoto kutoroka kwao nakua mtoto wa mitaani . Uongozi wa mtaa uliweze kumpeleka mtoto huyo Polisi na baba yake alifikishwa Mahakamani " anasema Sabato.

    Utunzaji wa Mazingira

" Uongozi wa mtaa uliungana na ofisi ya mkuu wa Wilaya wa Tarime kwenye Kampeni ya Tarime ya Kijani ambapo mtaa wetu tulipokea miche 400. 

       Mwenyekiti wa mtaa wa Sabasaba Sabato Marwa akipanda mti

"Miche hiyo ilipandwa shule tatu za  msingi, Kanisa la SDA na ofisi ya CCM wilaya ambapo pia baadhi ya wananchi mmoja mmoja walipata miche kwenda kupanda maeneo yao ya nyumbani kwao" anasema.

    Changamoto 

Palipo na mafanikio hazikosekani changamoto, mtaa huo wa Sabasaba hauna eneo la wazi la serikali jambo ambalo limesababisha mtaa kuendelea kupanga kwenye majengo ya watu binafsi.

" Mtaa wetu hauna eneo la wazi hata ofisi ya mtaa tumepanga chumba jengo la mtu binafsi.  Tunao mpango wa kujenga ofisi katika eneo la shule moja kati ya hizi shule tatu.

"  Mchakato umeishaanza ambapo mkutano mkuu wa mtaa ulishakaa na wananchi na kuhazimia ofisi Ijengwe katika moja ya shule zetu, tunangojea mamlaka ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji Tarime katika utekelezaji wa ombi letu na tunaishukuru serikali kwa mambo inayofanya ya kuwaletea wananchi maendeleo" anasema Sabato.

Anaiomba serikali kuwalipa fidia wananchi wanaoishi jirani na shule na kisha ijenge ghorofa kwani shule tatu zilizopo mtaani hapo zina eneo dogo na hazina viwanja vya michezo.

Pia anaiomba Serikali kuhakikisha huduma ya maji ya bomba inapatikana wakati wote ili kuwezesha mahitaji ya wananchi katika mtaa huo ambao upo mjini Tarime.

Anasema kwamba maji yamekuwa yakikatika mara kwa mara ,wakati mwingine hukaa zaidi ya siku tatu bila kutoka jambo  linaloleta usumbufu kwa wananchi.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Sabasaba.

Picha za matukio mbalimbali .











No comments