HEADER AD

HEADER AD

UWT YAWASISITIZA WANAWAKE KUJITOKEZA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Na Ada Ouko, Musoma

KATIBU mkuu wa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Mara , Zeydani Mwamba ametoa wito kwa Wanawake mkoani humo kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo udiwani, ubunge na nafasi ya viti maalumu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika , Octoba , 2025.

Zeydani ameyabainisha hayo Mei ,18 mwaka huu ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika Manispaa ya Musoma wakati akizungumza na wanawake wa chama hicho.

Katikati ni katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi Zeydani Mwamba akiwashukuru wajumbe wa UWT hawapo pichani kwa kushiriki mkutano wa kuwahamasisha kushiriki kuwania nafasi za udiwani, ubunge ngazi ya kata,katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu 2025

" Mfano mzuri ni uchaguzi mdogo uliopita zilitokea kata mbili za kujaza kata ya Mshikamano na kata ya Mwisenge, tuliwahamasisha akina mama tukawaondoa uwoga.

" Tukawaambia washiriki bahati nzuri walishiriki na tukapata kata moja ya Mwisenge , aligombea mwanamke na akashinda tayari ni diwani wa kata hiyo" amesema " Zeydani.

Zeydani amesema zoezi hilo linaendelea kufanyika akisaidiana na sekretarieti ya UWT mkoani hapa lengo likiwa ni kuondoa mfumo dume uliokuwepo mwanzo miongoni mwa wananchi.

       Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) wakiwa kikaoni.

 Sambamba na hilo aliweka wazi mabadiliko ya kanuni ya CCM kubadilisha mfumo wa wajumbe wanaoshiriki vikao vya maamuzi.

Naye Katibu wa UWT wilayani ya Musoma, Teddy Mageni amesema kuelekea uchaguzi mkuu chama hicho kimepokea maelekezo juu ya zoezi zima la uchaguzi huo na kwamba UWT mkoani humo imedhamiria kutoa kura za heshima na za mfano kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT) wakiwa kikaoni.

" Mama Rais Samia Suluhu Hassan ni mwanamke wa UWT ,  Musoma mjini tunaenda na mama Samia tutampa kura za heshima, mwaka huu 2025 tunataka tutoe kura za mfano kwa mwanamke mwenzetu" anasema Teddy.

Aliwahimiza wanawake na akina mama mkoani humo kujitokeza kwa wingi na kuchukua fomu ya kushiriki uchaguzi huo ifikapo tarehe 28 , June mwaka huu 2025,  kugombea nafasi ya udiwani, ubunge na viti maalumu kuanzia ngazi ya kata na wilaya kwa ujumla . 


      Katibu wa UWT mkoa wa Mara Zeydani Mwamba


     Wajumbe wa UWT wakimkabidhi Katibu wa UWT mkoani Mara keki

No comments