MNYEKE NA SADAKA YA NGO'MBE 2000 KONDOA
MWENYEZI namshukuru, kwa Ngo'mbe kuwachinjia,
Sikuifanya kufuru, nimezichinja kwa nia,
Wakazi nawashukuru, kwa nyama kujipatia,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumezichinja.
Kwingineko Tanzania, ni Ngo'mbe elfu nane,
Watu wamefurahia, tena ni Ngo'mbe wanene,
Huduma imeenea, subirieni mengine,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumewachinja.
Wengi wamesaidika, kwa nyama kujipatia,
Nimepambana hakika, zoezi kusimamia,
Kaniwezesha Rabuka, Mnyeke kanijalia,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumewachinja.
Sikuwachinja kwa ria, watu hilo tambueni,
Nimewachinja kwa nia, kwa watu kuwathamini,
Wengine wamechukia, nayasema si utani,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumewachinja.
Nimechinja kwa imani, kwa watu kusaidia,
Kaniwezesha Manani, malipo natarajia,
Nayasema kwa yakini, nimewachinja kwa nia,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumewachinja.
Kuchinja nawahusia, Idi ikitufikia,
Mwenyezi katuhusia, kuraani kupitia,
Chinjeni kwa wenye nia, thawabu kujipatia,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumewachinja.
Mwishoni naelekea, tukutane na mwakani,
Atupe afya Jalia, atujalie imani,
Mengi nimeelezea, tuyaweke akilini,
Ni Ngo'mbe elfu mbili kondoa tumewachinja.
SirDody(Mudio Islamic seminary)
Kilimanjaro
0675654955, au 0762396923.
Post a Comment