TWAJIVUNIA TANZANIA, TWAJIVUNIA KUWA WATANZANIA
NCHI yetu ya thamani, kwa jina ni Tanzania,
Jina lake la thamani, twapenda kulisikia
Nchi inatuthamini, na inatujali pia
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Tuna mbuga za wanyama, serengeti na manyara
Wapo pia kina duma, na wale kina sungura
Twaipenda Tanzania nchi tuliyozaliwa
Tunayo pia milima, Tanzania inang'ara
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Mabonde twajivunia, hakika yanavutia,
Maua yanachanua, asali twajipatia
Maua yananukia, porini yameenea
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Tanzania yapendeza, wa nchi waitamani
Kwa amani yaongoza, ulaya na duniani,
Ninapenda kuwajuza, Tanzania ya thamani
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Mlima wenye thamani, ni mrefu Afrika
Wasikika duniani, kwa urefu si utani
Kilimanjaro jamani, mlima twauthamini
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Bendera inapepea, amani kuashiria
Rangi zake zavutia, kijani na njano pia
Nyeusi twajivua, ni sisi Watanzania
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Kituoni nimefika, hongera Watanzania,
Twajivunia hakika, nchi yetu Tanzania
Twaishi bila mashaka, nchi tunajivunia
Twaipenda Tanzania nchi yetu ya thamani
Kutoka Kilimanjaro Tanzania
Najivunia kuwa Mtanzania
SirDody Dody Kilimanjaro
0762396923 au
0675654955
Post a Comment