WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA, MIAKA 30 JELA KWA KOSA LA UBAKAJI NA ULAWITI
Na Alodia Dominick , Bukoba
MAHAKAMA ya wilaya ya Bukoba, mkoani Kagera imewahukumu watu watatu, wawili kifungo cha maisha na mmoja miaka 30 kwa makosa ya ubakaji na ulawiti.
Wakili wa serikali Amon Mang’era ameeleza hayo Juni 02, 2025 wakati akiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ofisini kwakwe mjini Bukoba ambapo amemtaja, Rweyemamu Kashuja maarufu kama baba P bodaboda (35) mkazi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Amesema ametiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Bukoba kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka sita baada ya mahakama hiyo kulidhika na ushahidi wa upande wa Jamhuri pasipo kuacha shaka.
“Kati ya mwezi Aprili na Mei mwaka jana mshitakiwa Rweyemamu Kashunja (35) alimlawiti mtoto wa miaka mitano kwa wakati huo ambapo kwa sasa ana umri wa miaka sita na wakati shauri likiendelea mtuhumiwa na mdhamini wa kwanza ambaye ni mke wake walitoroka.
Amesema kesi iliendelea ambapo Mei 30 mwaka huu mahakama ilitoa hukumu na kumtia hatiani kwa kufungwa jera maisha kutokana na kifungu cha 154(1) (a) na (2) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo 2022” ameeleza
Amesema mshitakiwa Rweyemamu na mke wake Anchira Gozibart ambaye ni mdhamini wa kwanza wanatafutwa na mahakama ili wakatumikie adhabu zinazowakabili huku mdhamini wa pili aitwaye Nelson Mutagaywa akiendelea kutumikia kifungo cha nje cha miezi sita.
Amesema katika shauri hilo pia lilihusisha watoto wawili ambao walitenda kosa la ulawiti kwa mtoto huyo mwezi Desemba mwaka jana ambapo walikiri kosa na mahakama kutoa adhabu kulingana na sheria ya mtoto sura ya 13 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ambapo wamepelekwa ustawi wa jamii ili kupewa ushauri nasaha na uangalizi.
Pia mahakama hiyo imemhukumu Abdul Selemani (30) mfanyabiashara wa samaki mkazi wa Bukoba kwenda jera maisha baada ya kumbaka mtoto wa miaka saba.
Mang’era amesema hukumu hiyo ilitolewa Mei 28 mwaka huu, mshitakiwa ametiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha pasipo na shaka kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.
Imeelezwa kwamba Abdul alimbaka mtoto huyo kwa mara tatu mfululizo hivyo kutokana na kanuni ya adhabu kifungu cha sheria namba 131 (3)sura ya 16 marejeo ya 2022 na cha kosa 130 (1) na (2)e ambavyo ameshitakiwa navyo.
“Kati ya mwezi Aprili na Mei , mwaka jana mshitakiwa Abdul alimchukua mtoto huyo wa miaka saba wakati akitoka shule na kumuingiza ndani ya jumba chakavu ambalo haishi mtu na kumbaka mara tatu kwa nyakati tofauti ambacho ni kitendo cha kinyama na kwamba dada wa kazi aligundua tatizo hilo na kisha kumjulisha mama wa mtoto ndipo hatua zikachukuliwa” ameeleza Mang’era.
Katika tukio jingine mshitakiwa katika mahakama ya Wilaya Bukoba, imemhukumu kwenda jera miaka 30 Valentine Buberwa (41)mkazi wa Manispaa ya Bukoba maarufu kama baba mzazi kwa kosa la kumbaka mtoto wa jirani yake mwenye umri wa miaka mitatu.
Wakili Mang’era amesema tukio hilo lilitokea Oktoba, 25 mwaka jana ambapo mshitakiwa aliwakuta watoto watatu wakicheza na kumchukua mmoja ambaye ni mhanga na kumuingiza ndani ya nyumba yake alimokuwa akiishi mwenyewe.
Imeelezwa kuwa mshitakiwa alimbaka na kwmaba ndugu wa mhanga waliamua kufuatilia na kumkuta Valentine akiendelea kumbaka ndipo walipiga kelele zilizosababisha mshitakiwa kukamatwa.
“kutokana na ushahidi uliotolewa na Jamhuri mahakama imelidhika pasipo shaka na mwezi Mei , 30 mwaka huu ilitoa hukumu na kumtia hatiani mshitakiwa Valentine kufungwa miaka 30 jera kutokana na kifungu cha sheria namba 131 (3) sura ya 16 marejeo ya 2022”.
Mang’era amesema kesi zote zilisikilizwa mbele ya hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama ya Wilaya ya Bukoba Flora Kaijage na kijiridhisha na ushahidi uliotolewa na mashaihidi upande wa Jamhuri pasipo shaka na kisha kutoa hukumu hizo wka washitakiwa zilizowatia hatiani.
Post a Comment