HEADER AD

HEADER AD

WAFANYABIASHARA KAGERA WASEMA BAJETI YA SERIKALI IMEWAGUSA WAFANYABIASHARA


Na Alodia Dominick, Bukoba

BAADHI ya wafanyabiashara mkoani Kagera wamesema kuwa, bajeti ya serikali ya mwaka 2025/2026 imegusa maeneo mengi ya wafanyabiashara na wanatarajia bajeti hiyo itapunguza kero walizokuwa nazo.

Wafanyabaishara hao wameyasema hayo June 16, 2025 wakati wakizungumza na DIMA Online ambapo wameeleza kuwa, kutokana na bajeti iliyosomwa Bungeni June 12, 2025 na Waziri wa fedha hapa nchini Mwigulu Nchemba imegusa maeneo mengi ya wafanyabiashara na wanatarajia changamoto walizokuwa nazo zitapungua.

Ramadhan Makule ni mfanyabiabaishara wa mazao na mmiliki wa hotel kutoka wilaya ya Ngara mkoani hapa amesema kuwa, bajeti ya serikali imeonyesha kuwajali wafanyabiashara kwani malalamiko yao kwa asilimia kubwa yamefanyiwa kazi.



Amesema wabunge ambao ndiyo wako karibu na jamii waone kile ambacho hakijaguswa na serikali wakiguse ili wafanyabiashara waendelee kupata unafuu maana wafanyabiashara wana nafasi kubwa kwani wanaongeza kipato cha nchi kupitia ulipaji kodi.

“Serikali haiwezi kuendeshwa wakati wafanyabiashara wanalalamika lakini wafanyabiashara wakifurahi mambo yatakuwa mazuri tutalipa kodi na hakuna kitu ambacho kitakwama” amesema Makule

Akizungumzia wawekezaji /wafanyabiashara wa nje ya nchi amesema kuwa, katika bajeti wameangaliwa wachina waliopo Kariakoo lakini mkoa wa Kagera maeneo ya mpakani  wafanyabiashara wengi wanafanya baishara za mazao.

" Serikali isiangalie sehemu moja ya Wachina bali iangalie pande zote za wafanyabiashara na waone wao kama wafanyabiashara  wa ndani wanawalindaje kuweza kufanya biashara zao za mazao na biashara nyingine ndogo ndogo

      Wa kwanza  kulia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara kanda ya ziwa na   mkoa wa Kagera Nicholaus Basimaki akitoa maoni kuhusu bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026 kulia kwake ni katibu wa Jumuiya hiyo Phinias Bashaya.

Avelina Theonest ni mfanyabiashara wa nafaka mjini Bukoba ameishukuru serikali katika bajeti iliyosomwa kwamba imelenga kutatua changamoto za wafanyabiashara kwani walikuwa na kero ya kufungiwa biashara zao.

Amesema wanaamini baada ya bajeti kusomwa wameona iwapo sheria inayowapa mamlaka serikali za mitaa itaondolewa watafanya biashara zao bila usumbufu.  

Amesema serikali iendelee kutatua changamoto za wafanyabiashara ili kuweka unafuu kwao wa kuweza kufanya shughuli zao kwa uhuru.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Kanda ya ziwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Kagera Nicholaus Basimaki amepongeza jitihada za serikali maana bajeti imegusa maeneo mengi ya wafanyabiashara na itapunguza kero kwao.

“Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameelekeza wasaidizi wake waweze kusikiliza changamoto za wafanyabishara.

 " Tumeona kwenye bajeti yameainishwa mambo mbalimbali mfano sheria ya fedha ya serikali za mitaa sura ya 290 ambayo ni hotuba iliyotolewa na Waziri wa fedha inapendekeza ifanyiwe maboresho”amesema Basimaki

Ameeleza kuwa wafanyabiashara wanaunga mkono kwamba katika maeneo hayo hasa kwenye maeneo ya tozo na ushuru mfano ushuru wa huduma ambayo ilikuwa ikitozwa kwenye mauzo ghafi 0.3 itakwenda kutozwa kwenye faida kwa maana ya pato ghafi. 



Ametaja eneo jingine lililopewa unafuu ni kwenye hotel levi (ushuru wa hotel) ambao ulikuwa unakokotolewa kwenye mauzo baada ya kuondoa matumizi unatoa asilimia 10 na hii itaondoa kero kwa wawekezaji wa hotel, nyumba za wegeni  na wafanyabiashara.

“Ilikuwepo kero ya wafanyabiashara kufungiwa maduka bila kusubili mtu anafika anafanya ukaguzi hapo hapo anafunga maduka sasa na tunaona pendekezo hili likipitishwa kwenye mswada wa sheria itasaidaia kuondoa kero ambazo zitaweza kuongeza tija na mazingira mazuri ya ufanyaji biashara.

" Wafanyabiashara watajiamini na watakuwa na muda wa kufanya bishara bila mawazo ya kufungiwa na sisi tunasema mapendekezo haya yapitishwe na mswada huu usainiwe iwe sheria” amesema Basimaki.

Amesema wanakubaliana na mapendekezo ya Waziri wa fedha kwenye mswada wa sheria ushuru wa kupakia na kushusha ufutwe kama ilivyopendekezwa na katika misamaha iliyotolewa kwenye mali ghafi/bidhaa za kuongeza uzalishaji pia mapendekezo hayo yaendelee.

Aidha ameiomba serikali kutatua changamoto kwenye maji kwani walitegemea tozo inayotozwa kila lita ya maji sh. 46 ipunguzwe hadi sh.10 ili kuwezesha viwanda vya maji hasa vidogo kuendelea kuongeza uzalishaji ili waendelee kushindana na viwanda vikubwa.

No comments