MAMA NI WA KIPEKEE

MAMA ni mama, jamani,
Eti nani, anabisha,
Anapepea nchini, Tanzania heshimisha,
Hawezi kupigwa chini, mengi ametufundisha,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Barabara tengeneza, twatembea kwa amani,
Hakika anapendeza, kutuongoza nchini,
Wala hapendi ongoza, kwa matabaka jamani,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Mbali ulipotutoa, paka Leo tumefika,
Ahsante mama Samia, twakupa zote baraka,
Watu tutakuchagua, tena usiwe na shaka,
Nahakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Wewe wetu kiongozi, sisi twakutegemea,
Usije kutoa Mbuzi, watu hongo wapatia,
Wala kuleta mavazi, raia kuongopea,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Sote tuige mfano, kwa wetu mama Samia,
Tulete mshikamano, Samia kumchagua,
Hakika yeye ni mfano, Tanzania endelea,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Tuna philipo mpango, mama kumsaidia,
Wapanga mingi mipango, Tanzania kuinua,
Wanaepuka kwa hongo, masikini saidia,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Mama Samia mwerevu, raia kusikiliza,
Tena tuache uvivu, yeye anasisitiza,
Nasi tusiwe wabovu, uvivu utatuponza,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Ushindi kujishindia, ondoa kabisa shaka,
Raia kusaidia, kukamata na vibaka,
Mtaani kutishia, waiba hadi mapaka,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
Mwisho kwa kumalizia, Sina mengi ya kusema,
Ushindi utachukua, usimame kama mama,
Rushwa usije pokea, itaturudisha nyuma,
Na hakika kwa yakini ushindi wako kabisa.
*SirDody*(Mudio Islamic seminary)
_Kilimanjaro_
0675654955
Hujalichapisha hili
Post a Comment