TUMEPOKEA KWA MASIKITIKO MSIBA WA SHOMARI BINDA
WANAHABARI poleni, kwa msiba kuwafika,
Imekuwa ni huzuni, kwa mwenzetu kututoka,
Ni vigumu kuamini, kama kweli katutoka.
Shomari Binda kwa heri ulazwe mahali pema.
Umeondoka haraka, simanzi metuachia,
Tuna uchungu hakika, Shomari twakulilia,
Nyoyo zinahuzunika, kifo tukifikiria,
Shomari Binda kwa heri ulazwe mahali pema.
Wewe umetangulia, muda wako umefika,
Na sote tutarejea siku yetu ikifika,
Hakuna wakubakia, tutakufa kwa hakika,
Shomari Binda kwa heri ulazwe mahali pema.
Mwendo umeumaliza, kwa Mola unarejea,
Sisi tutaomboleza, kwa dua kukuombea,
Msiba tutatangaza, nchini utaenea,
Shomari Binda kwa heri ulazwe mahali pema.
Mwishoni naelekea, nina uchungu moyoni,
Ukingoni nafikia, wafiwa wote poleni,
Mengi nimeelezea, msiba kuuthamini,
Shomari Binda kwa heri ulazwe mahali pema.
SirDody (Mudio Islamic seminary)
Kilimanjaro.
0675654955
Post a Comment