WANA CCM 213 WAUSAKA UDIWANI TARIME
>> Wamo wanawake 30
>> Wote wafukuzia kata 34
Na Dinna Maningo, Tarime
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilayani Tarime, mkoani Mara, wapatao 213 wamerejesha fomu wakiomba kuteuliwa kugombea udiwani katika kata 34 .
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) wilaya ya Tarime , Hamza Adam Kyeibanja, amesema kwamba katika halmashauri ya wilaya ya Tarime waliochukua fomu kuwania udiwani ni wanachama 165 kati yao wanaume ni 143 na wanawake 22.
Amesema wote wamerejesha fomu ambapo katika halmashauri ya mji wa Tarime, waliochukua fomu ni wanachama 50, kati yao wanaume ni 42 na wanawake ni 8.
Waliorejesha fomu ni 48 kati yao wanaume 40 na wanawake 8 na kwamba kwa sasa vinafanyika vikao vya mchujo huku akiongeza kwamba hali ni shwari.
Kwa mujibu wa ratiba ya chama cha Mapinduzi ( CCM), tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu ni kuanzia tarehe 28/06/2025 mpaka tarehe 02/07/2025.
Kuteua majina matatu (03) ya wagombea ubunge na udiwani wa Kata ni tarehe 09/07/2025 mpaka tarehe 19/07/2025.
Kujitambulisha kwa wagombea ubunge wa majimbo kwenye Kata na wagombea Udiwani kata ni kuanzia tarehe 27/07/2025 mpaka tarehe 01/08/2025.
Zoezi la kupiga kura za maoni ndani ya chama ni tarehe 02/08/2025 kwa wagombea udiwani wa kata na ubunge wa majimbo kwenye kata.
Uteuzi wa wagombea (mmoja mpeperusha bendera wa chama) Udiwani wa kata ni tarehe 11/08/2025.
Uteuzi wagombea (mmoja-mpeperusha bendera wa chama) Ubunge kila jimbo ni tarehe 20/08/2025 ambao ndio watakaogombea kuchuana na wagombea wengine wa vyama vya upinzani ili kupigiwa kura na wananchi katika uchaguzi mkuu, utakaosimamiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ( INEC ) utakaofanyika mwaka huu.
Post a Comment