KIFO CHA SPIKA MSTAAFU JOB NDUGAI
JOB Yustino Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Taifa la Tanzania, Job Yustino Ndugai amefariki dunia tarehe 6, Agosti 2025 mjini Dodoma, akiwa katika matibabu.
Taarifa hiyo imetolewa rasmi na Spika wa sasa, Dkt. Tulia Ackson . Amefariki akiwa na umri wa miaka 62 .
Mazishi
Taarifa kutoka ofisi ya Spika ilisema kwamba Ofisi ya Bunge kwa ushirikiano na familia ya marehemu pamoja na kamati ya mazishi inayoongozwa na Serikali, wanaendelea kupanga ratiba rasmi ya mazishi .
Spika Tulia , amesema Jumapili, tarehe 11 Agosti 2025, mwili wake utapelekwa kwenye Viwanja vya Bunge, kabla ya kusafirishwa na kuzikwa nyumbani kwake Kongwa .
Ndugai aliyekuwa mtiania na akitetea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo alikuwa ameshinda kura za maoni katika uchaguzi wa kura za maoni katika Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika Agosti, 04, 2025.
Historia ya Utumishi na Uongozi
Inaelezwa kwamba Ndugai alizaliwa Januari 21, 1963, Tanganyika (sasa Tanzania) Elimu | |
Alipata elimu ya awali na sekondari nchini, akajikita katika elimu ya juu; Diploma (Mweka), BSc (UDSM), MSc (Agricultural University of Norway), na hata shahada ya sheria LLB (Open University of Tanzania). Siasa | |
Amekuwa mbunge wa Kongwa tangu mwaka 2000 hadi kifo chake mwaka 2025 | |
Kuanzia Novemba 2010 hadi Novemba 2015 | |
Aliteuliwa kuwa Spika Julai 17, 2015, na akateuliwa tena mwaka 2020. Alijiuzulu rasmi tarehe 6 Januari 2022, alipoondoka kwa hiari katika wadhifa huo. Job Yustino Ndugai | |
Alijulikana kwa msimamo thabiti juu ya uwajibikaji serikalini, nidhamu ya bunge, na aliibuka kama kiongozi tajiri wa uzoefu. Athari na msimamo Wakati wa utumishi wake kulizuka mjadala kuhusu hatua zake bungeni, ikijumuisha mgogoro wa deni la taifa na suala la wabunge wa vyama vya upinzani. |
Kifo cha Job Ndugai ni pigo kubwa kwa siasa za Tanzania, kiongozi aliyejitolea kwa miaka nyingi katika huduma ya umma. Mazishi yake yameandaliwa kwa heshima, yakiwa ni siku ya mwisho ya kumkumbuka rasmi, kabla ya mwili kuzikwa nyumbani kwake Kongwa.
Post a Comment