BURIANI SPIKA WA BUNGE MSTAAFU JOB NDUGAI
NYOYO zinahuzunika, zimengiwa fedhehani,
Kwa mhebi kututoka, naeleza si utani,
Mola amemuitika, hako tena duniani,
Mola muweke peponi mpendwa wetu ndugai
Habari zimesikika, za kifo chake jamani,
Ni huzuni kwa hakika, majonzi tele moyoni,
Bado ulihitajika, ni kubwa yako thamani,
Mola muweke peponi mpendwa wetu ndugai.
Pumzika kwa amani, sisi tunakulilia
Waondoka duniani, warejea kwa jalia,
Tutakuja mazikoni, huku tukikulilia
Mola muweke peponi mpendwa wetu ndugai
Mwishoni nimefikia, kwa uchungu ninalia,
Nashindwa kuelezea furaha imepotea
Shairi ninalitoa, hakika nimeumia,
Sirdody
0675654955/ 0762396923.
Post a Comment