HEADER AD

HEADER AD

MPINA ALIYEKUWA CCM AJIUNGA ACT NA KUIDHINISHWA KUWA MGOMBEA URAIS

CHAMA cha ACT Wazalendo kimemuidhinisha rasmi Luhaga Mpina , aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)  na kisha kuhamia ACT, kuwa mmoja wa wagombea wa Urais atakayechuana na Rais Samia Suluhu Hassan wa CCM kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2025.

Uamuzi huo umefikiwa na Halmashauri Kuu ya ACT wazalendo jijini Dar es Salaam, ambayo ilipendekeza majina mawili, Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.

            Ruhanga Mpina aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kisesa kupitia chama cha CCM na kuhamia ACT Wazalendo.

Majina hayo yaliyopendekezwa yaliwasilishwa kwa Mkutano Mkuu Taifa kwa ajili ya kupigiwa kura, ambapo katika mkutano huo, Mpina alichaguliwa kwa kishindo kwa kupata kura 559 sawa na asilimia 92.3 ya kura zote 610 zilizopigwa.

Luhaga Mpina amemshinda Mgombea mwenzake Kalikawe aliyepata kura 46 sawa na asilimia 7.7 na sasa atapeperusha bendera ya ACT katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, mgombea mwenza akiwa Bi. Fatma Ferej.

Kwa upande wa Zanzibar, Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Othman Masoud Othman amechaguliwa kuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupata kura 606 za ndiyo sawa na asilimia 99.5 ya kura zote halali 609.

Luhaga Joelson Mpina alikuwa mbunge wa Jimbo la Kisesa. Mwaka 2005 alichaguliwa mara ya kwanza kuwa mbunge akarudishwa katika chaguzi za 2010, 2015 na 2020.

Amewahi kushika nafasi kadhaa za kisiasa ikiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano M

Luhaga Mpina kati ya mwaka 2015-2017, baadaye mwaka 2017 - 2020 alikuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika serikali ya rais John Magufuli.

Mpina amekuwa pia mjumbe kwenye kamati mbalimbali za bunge ikiwemo ya fedha na uchumi, viwanda na biashara na kamati ya bajeti.

Mpina ambaye ni mtaalam wa fedha ana shahada kwenye sekta hiyo, moja akipata Chuo kikuu cha Dar es Salaam na nyingine chuo kikuu cha Strathclyde nchini Uingereza.

Ameshawahi kufanya kazi kama mtendaji wa kata huko Meatu, mwaka 1999-2000 na mhasibu wa daraja la pili.

Kwenye chama chake cha zamani, CCM, Mpina amewahi kuwa mwenyekiti wa Umoja wa vijana (UVCCM) Meatu kwa miaka 5 kati ya 2003 mpaka 2008.

Mkosoaji asiyeogopa

Mpina amekuwa mkosaji mkubwa bungeni na nje ya bunge. Akizungumza bungeni ama nje usingedhani kama anatoka chama tawala cha CCM, ungedhani ni mpinzani kutoka vyama vya upinzani.

Aliwahi kusema haogopi kukosoa, kwa sababu anaamini anatekeleza wajibu wake kama mbunge na muwakilishi wa wananchi, akitetea kwamba Mbunge si kupiga makofi na kupongeza pekee, bali kazi ya msingi ni kuishauri serekali pale inapokosea.

Mwaka 2024 alifungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu Masjala ya Dar es Salaam dhidi ya Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe, Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, Bodi ya Sukari na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mpina alikuwa anapinga uamuzi wa Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe kutoa vibali vya ununuzi wa Sukari kupitia Bodi ya Sukari kwa kampuni ambazo hazimiliki Viwanda vya Sukari wala Biashara ya Sukari.

Aidha Mpina katika madai yake pia alikuwa anapinga Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kuruhusu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania "TRA" kuruhusu Kampuni za vocha kuingiza Sukari nchini bila kulipa kodi na kuisababisha Serikali hasara ya Shilingi Bilioni 1.548.

Mpina alikuwa mkosoaji wa masuala ya kitaifa kuanzia sakata la wizi wa mabilioni ya fedha za Escrow mpaka sasa kwenye masuala ya sukari. Na kwa kuwa hakukuwa na nguvu kubwa ya upinzani bungeni, ukosoaji wake bungeni uliangazwa zaidi na wengi.

Kwenye moja ya ziara ya Rais Samia, jimboni Kisesa hivi karibuni, Mpoina bila woga alisema wananchi wa Kisesa tunakudai', akifikisha ujumbe wa ukosoaji wa 'staha' kwa rais kwamba kuna mambo mengi hajatimiza kwenye jimbo hilo.

Rais Samia alimjibu kwenye mkutano huo huo mbele ya wananchi wake akisema "ni kujitafutia umaarufu, hakulifanyia haki jimbo lake', akimtaja piamkama mbunge wa taifa na sio mbunge wa kupigania jimbo lake.

Kauli ya Mpina na majibu ya rais, yalitoa picha ya wazi kuwa siku za mbunge huyo kuongoza jimbo hilo zilikuwa zinahesabika.

Ni kweli, jina lake liliondolewa na vikao vya juu huku majina saba yakipitishwa kugombea nafasi hiyo, kama ilivyotarajiwa na wengi. Hatua ya kutomrejesha ikaibua tafsiri tofauti kuhusu mwelekeo wa chama kuelekea uchaguzi mkuu huu.

Agosti 6, 2025 akatangazwa kuhamia ACT baada ya kuthibitishwa na vikao vya Agosti 5.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuhamia ACT sasa amepata uwanja mpana wa kukosoa kwa uhuru zaidi.

Mbunge wa kitaifa

CHANZO : BBC

No comments