CCM PWANI YATANGAZA MATOKEO YA UBUNGE KURA ZA MAONI
Na Gustaphu Haule, Pwani
KATIBU wa Siasa ,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Pwani David Mramba ametangaza matokeo ya uchaguzi wa kura za maoni uliofanyika Agosti 4,2025.
Mramba ametangaza matokeo hayo mbele ya Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika mkutano uliofanyika ofisi ya CCM Mkoa wa Pwani Agosti 5,2025.
Mramba ametangaza matokeo ya Jimbo la Kibiti ambapo alisema Jimbo hilo lilikuwa na wagombea watatu huku idadi ya wapiga kura ni 10,277 na kura zilizopigwa 7007.
Kura zilizoharibika 137 na kura halali ni 6870 na aliyeongoza ni Amina Musa Mkumba aliyepata kura 4,712,Kharid Mtalazaki amepata kura 1102, na Ally Seif Ungando 1068.
Katika jimbo la Rufiji Mramba amesema kura zilizopigwa ni 8,534 ,zilizoharibika 1, na kura halali 8,533 ambapo Hamisi Kisoma amepata kura nane,Salum Ponga amepata kura 34 , Selemani Muekela amepata kura 26, na Mohamed Mchengerwa ameongoza kwa kupata kura 8,465.
Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Pwani David Mramba akitangaza matokeo ya uchaguzi wa ubunge kura za maoni uliofanyika Agosti 4,2025.Jimbo la Mafia amesema kura zilizopigwa ni 2,628 ,kura zilizoharibika 60 na kura halali ni 2,568, wagombea walikuwa wanne akiwemo Omary Kimbau aliyepata kura 614,Mbaraka Dau aliyepata kura 759, Amina Tuki (09) na Omary Kipanga ameongoza kwa kupata kura 1,186
Kuhusu Jimbo la Mkuranga amesema kulikuwa na wagombea watano ambapo Gift Mipiko (440), Mohamed Kilalile (4,293),Mwasiti Matola (180),Prisca Ngweshem (22) na Abdallah Ulega ameongoza kwa kupata kura 8,490.
Jimbo la Kisarawe idadi ya wagombea walikuwa watano,idadi ya kura zote ni 5828 ,kura zilizopigwa ni 5,105 ,kura zilizoharibika 170, kura zilizokataliwa 7 na kura halali ni 4,936.
Ally Janguo amepata kura (164), Msafiri Mpendu (804),Salum Chaurembo(321),Tabia Kalega (117) na aliyeongoza ni Selemani Jafo aliyepata kura 4,412.
Katika Jimbo la Kibaha Mjini amesema kulikuwa na wagombea Sita na kura zilizotakiwa ni 6,300 ,kura zilizopigwa ni 5,743,kura zilizoharibika ni 53 na kura halali ni 5,682.
Ibrahimu Mkwillu amepata kura (35), Magreth Mwihava (39),Dkt.Charles Mwamwaja amepata kura (282), Abubakar Allawi (727),Musa Mansour (1,775) na aliyeongoza ni Silvestry Koka aliyepata kura 2,824.
Aidha,Jimbo la Kibaha Vijijini kulikuwa na wagombea watatu ambapo kura zilizotakiwa ni 6,215,kura zilizopigwa 5,300,kura zilizoharibika 83,kura halali ni 5,227.Heri Paulo amepata kura (176), Michael Mwakamo (1,802) na aliyeongoza ni Hamoud Jumaa aliyepata kura 3,247.
Katika Jimbo la Chalinze amesema mgombea alikuwa mmoja ambaye ni Ridhiwani Kikwete na kura zilizotakiwa ni 12,074 lakini kura zilizopigwa ni 12,245 na kura zilizomkataa 171.
Jimbo la Bagamoyo Mramba amesema kulikuwa na wagombea watano na idadi ya kura zilizopigwa ni 5,567,kura zilizoharibika ni 232,kura halali ni 5,535 ambapo Mathias Kambi amepata kura 37, Haji Ngwila 47, Christina Henry amepata kura 133,Mwarami Mkenge amepata kura 1,574 na Subira Mgallu ameongoza kwa kupata kura 3,544.
Post a Comment