HEADER AD

HEADER AD

TUONDOLEE MAZITO, DUNIANI NA AKHERA



TUNAKUOMBA  Manani, waja wako duniani,
Twakuomba kwa yakini,  tuipushe mitihani,
Utukinge na shetani, kama ulivyomlani, 
Yaillahi Mola wetu tuondolee mazito

Peponi twatarajia, waja wako kuingia,
Tuondoshee balaa,  tupe afya njema pia, 
Wewe tunakulilia, dhambi tufutie pia
Yaillahi Mola wetu tuondolee mazito.

Tujaalie imani, ya wewe kukutukuza,
Ututoe na dhambini, na mema kuendeleza, 
Twakuomba Rahamani, maisha yetu angaza,
Yaillahi Mola wetu tuondolee mazito.

Utupe amali njema, Utuepushe na dhima,
Mbele zako twasimama,  kuomba yako huruma,
Tuwie radhi karima,  utupatie na mema,

Shairi tunalitoa, mwishoni tumefikia,
Mengi tumeelezea, ipokee yetu dua,
Tumekuomba kwa nia, malipo twatarajia,
Yaillahi Mola wetu tuondolee mazito.

Sirdody
Soyakijijini@gmail.com
*0675654955*

No comments