MGOMBEA UBUNGE AAHIDI UMEME MAENEO YOTE JIMBO LA BARIADI MJINI
Na Abdallah Nsabi, Simiyu
MGOMBEA ubunge kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Bariadi mjini,mkoani Simiyu, Mhandis Andrea Kundo amewaahidi wananchi kwamba wakimpatia ridhaa ya kuwa mbunge atahakikisha maeneo yote ya Jimbo la Bariadi yanapata umeme.
Ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi katika mikutano ya kampeni kata za Guduwi, Bunamhala na Bariadi kwa nyakati tofauti.

Mhandisi Andrea amesema maeneo yote ya Jimbo hilo yakiunganishiwa umeme yatakuwa na maendeleo hivyo ni vyema wananchi wakakichagua chama cha CCM kwa kumpigia kura nyingi mgombea urais Dkt. Samia Suluhu, wabunge na Madiwani wa chama hicho.
Mkazi wa kata ya Guduwi Sitta Joshua, amemwomba mgombea ubunge huyo kushughulikia changamoto ya ukosefu wa umeme kwani utasaidia kuharakisha maendeleo.
Post a Comment