KARIBUNI SACODEA CHUO CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI DAR ESALAAM
KARIBU sacodea, mjipatie elimu,
Ni chuo cha famasia, chenye mahiri walimu,
Hakika kinavutia, twakiombea kidumu,
Karibuni sacodea elimu kujipatia.
Ni chuo chenye dhamira, vijana kuangazia,
Chasifika kwa ubora, wa elimu kuitoa,
Hakika ni chuo bora, vigezo chajivunia,
Karibuni sacodea elimu kujipatia.
Wanafunzi karibuni, yawangoja sacodea,
Jiungeni kwa yakini, ujuzi kujipatia,
Ni chuo chenye thamani, jina lake linakua,
Karibuni sacodea elimu kujipatia.
Majengo yake mazuri, madhari ya kuvutia,
Kimepangika vizuri, wengi kinawavutia,
Chuo hiki ni kizuri, mengi kinajivunia,
Karibuni sacodea elimu kujipatia.
Chapatikana nchini, jiji la Darisalama,
Wanafunzi jiungeni, sacodea ni salama,
Mtajipatia fani, imara mtasimama,
Karibuni sacodea elimu kujipatia.
Mwishoni nimefikia, shairi ninalitoa,
Mengi nimeelezea, kwa ujumbe kuutoa,
Wadau twawangojea, tena twawasubiria,
Karibuni sacodea elimu kujipatia.
Sacodea chuo cha Afya
Sirdody Dody
0675654955

Post a Comment