HEADER AD

HEADER AD

RAIS SAMIA AAGIZA VIJANA WALIOANDAMANA KWA KUFUATA MKUMBO WAACHIWE


RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza msamaha kwa vijana waliokamatwa kufuatia maandamano ya siku tatu yaliyofanyika kuanzia siku ya uchaguzi, Oktoba 29, 2025.

Akizungumza bungeni Novemba, 13, 2025 wakati wa kulifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Ibara ya 91(1) ya Katiba, Rais Samia amesema kuwa vijana hao wengine walifuata mkumbo hivyo waachiwe kwa utaratibu na kurejeshwa kwa familia zao.

''Vijana wengi waliokamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua wanachokifanya, nikiwa mama na mlezi wa taifa hili na vielekeza vyombo vya kisheria na hasa ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka kuangalia kiwango cha makosa waliyofanya, na kwa wale ambao hawakudhamiria kufanya uhalifu, wafutiwe makosa yao,'' amesema Rais Samia.

Maandamano hayo yaliripotiwa kusababisha vifo vya watu kadhaa, wengine kujeruhiwa, na uharibifu wa mali za umma na binafsi. Zaidi ya vijana 600 wwalikamatwa na kufunguliwa makosa yakiwemo ya uhaini.

Miongoni mwa waliokamatwa ni mfanyabishara Jenipher Jovin maarufu kama Niffer Pamoja na mashtaka ya njama za uhaini na uhaini pia anashtakiwa kwa uchochezi wa kuhamasisha umma kununua barakoa za kuzuia moshi wa kutoa machozi wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa Oktoba 29,2025.

Rais Samia pia alitangaza kuwa serikali imeunda tume maalumu kuchunguza matukio yaliyotokea wakati wa maandamano hayo.

"Serikali imechukua hatua ya kuunda tume itakayochunguza kwa undani kilichotokea ili tujue kiini cha tatizo. Taarifa ya tume hiyo itatuongoza katika mazungumzo ya kuleta maridhiano na kudumisha amani," 

No comments