HEADER AD

HEADER AD

MENEJA TARURA ALIYEKUWA AMESHIKILIWA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MKEWE AACHIWA , WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI


>>Waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji mmoja ni Mwalimu

Na Mwandishi Wetu, Musoma

MWALIMU anayefundisha shule binafsi ya msingi na Sekondari Mbalali, mkoani Mbeya , Marco Marco Maginga mwenye umri wa miaka 47 na Mwita Abel Maginga (45) mkazi wa wilayani Tarime, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na shtaka la mauaji ya Rodha Jonathani (42) mkazi wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Washtakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Musoma, Eligeria Rujwahuka ambapo wanadaiwa kutenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 196 na kifungu cha 197 cha kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023.

       Washtakiwa wakitoka mahakamani Musoma Desemba, 23,2025 kusikiliza kesi ya mauaji ya Rhoda Jonathani inayowakabili .

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba , 23, 2025 kwa kumuua Rhoda Jonathan Mobe mkazi wa Kijiji cha Burunga , Kata ya Uwanja wa Ndege wilayani Serengeti.

Kwa upande wa mashitaka, wakili wa serikali Joyce Matindwa, amesema kwamba shauri lililokuja kwa ajili ya kutajwa hali ya upelelezi bado haujakamilika.

Wakili Joyce ameiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya shauri hilo kutajwa.

Hakimu mkazi wa Mahakama hiyo, Eligenia Rujwahuka amesema shauri hilo halina dhamana na mahakama hiyo haina mamlaka zaidi ya kusubiri taratibu za upelelezi.


Wakili Linus Amri anayewakilisha wanafamilia na Ndugu wa marehemu ambaye yupo kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa kesi hiyo amesema tayali watuhumiwa wamefikishwa mahakamani lakini bado Jamhuri haijakamilisha upelelezi.

Anapendekeza upande wa Jamhuri kukamilisha upelelezi" wakamilishe upelelezi kwasababu ni kesi ambayo imeamsha hisia za watu kutokana na tukio la kikatili alilotendewa Rhoda ambaye kwa sasa ni marehemu baada ya kuaawa nyumbani kwake kwa kukatwa katwa mapanga.

      Wakili Linus Amri anayewakilisha wanafamilia na ndugu wa marehemu ambaye yupo kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa kesi ya mauaji ya Rhoda Jonathani.

Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Januari, 5, 2026 itakapotajwa tena na washtakiwa wamerudishwa rumande. Wakili wa washtakiwa hao wawili ni Mluge Karol .

>>>Rejea 

Oktoba, 26,2025 chombo hiki cha habari kiliripoti  habari yenye kichwa cha habari 'MKE WA MENEJA TARURA AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA SERENGETI. Oktoba, 26,2025 ikiripotiwa habari ' WAMUOMBA RAIS SAMIA, SERIKALI YA MARA KUWASAKA NA KUWAWAJIBISHA WALIOMUUA MKE WA MENEJA TARURA

Pia Oktoba, 27, 2025 chombo hiki cha habari kiliripoti habari ' FIDIA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE SERENGETI HUWENDA IKAWA CHANZO CHA KUONDOA MAISHA YA MKE WA MENEJA TARURA.

Oktoba 28,2025 iliripotiwa habari ' MWILI WA RHODA ALIYEUAWA KWA MAPANGA WAENDELEA KUSOTA MOCHWARI, NDUGU WAGOMA KUZIKA. Novemba, 7,2025 iliripotiwa habari ' SERIKALI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WALIOHUSIKA MAUAJI YA MKE WA MENEJA TARURA.

Awali Oktoba , 26, 2025 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara, Pius Lutumo, alisema kuwa Jeshi la Polisi mkoa wa Mara linamshikilia Wilson Mwita Charles mwenye umri wa miaka 52 mkazi wa Kitongoji cha Burunga , Kata ya Uwanja wa Ndege wilayani Serengeti na watu kadhaa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Rhoda Jonathani .

Kamanda Pius alisema kuwa baada ya uchunguzi wa awali Jeshi la Polisi mkoani humu linamshikilia Wilson Mwita Charles ambaye ni mume wa marehemu kwa ajili ya mahojiano zaidi ya tukio hilo. Waliofikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la mauaji ya Rhoda ni Mwita Abel na Marco Marco.

Familia ya marehemu akiwemo mama mzazi Ester Mobe waliiomba Serikali kutenda haki ili waliohusika kifo cha mwanae wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wengine nia ovu.

Wakazi wa Kitongoji cha Burunga , wilayani Serengeti walipozungumza na DIMA Online walimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati ili waliohusika na tukio hilo wachukuliwe hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wengine .

Mauaji ya Rhoda yalisababisha mwili wake kusota chumba cha kuhifadhia maiti kwa wiki mbili tangu kifo chake kitokee Oktoba, 23, 2025 ambapo familia ya marehemu walisema hawawezi kuzika hadi watakapopata taarifa za awali za uchunguzi wa kifo cha ndugu yao ikiwa ni pamoja na wahusika kufikishwa mahakamani.

Marehemu Rhoda alizikwa Novemba, 06, 2025 katika makaburi ya kanisa la Waadventista Wasabato wilayani Serengeti. Enzi ya uhai wake yeye na mmewe Wilson Charles ambaye ni Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) mkoani Kagera hadi mkewe anafikwa na mauti walifanikiwa kupata watoto watatu.

Kati ya watoto hao wawili ni wa kike na mmoja ni wa kiume mwenye umri wa miaka saba mwenye ulemavu wa viungo.

Mkuu wa wilaya ya Serengeti Angelina Lubela na mkuu wa wilaya ya Tarime Edward Gowele ni miongoni mwa walioshiriki mazishi ya Rhoda na kutoa mkono wa pole kwa familia Tsh. Milioni moja (1,000,000).

Mkuu wa wilaya ya Serengeti aliwahakikishia waombolezaji na familia ya marehemu kuwa serikali itahakikisha hatua zote za kisheria zinachukuliwa dhidi ya wote waliohusika na mauaji na kufikishwa mahakamani.






No comments