HEADER AD

HEADER AD

WATOTO 58 WAZALIWA TARIME MKESHA WA KRISMASI, WAKIUME NI WENGI KULIKO WA KIKE


Na Mwandishi Wetu , Tarime

JUMLA ya watoto 58 wilayani Tarime, mkoa wa Mara, wamezaliwa wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi, Desemba, 24, 2025. Kati yao jinsi ya kiume ni 32 na jinsi ya kike ni 26.

Akizungumza na DIMA online , Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Tarime , Dkt. Amin Vasomana amesema katika halmashauri ya wilaya ya Tarime wamezaliwa watoto 49 kati ya hao watoto wa kiume ni 27 na wakike ni 22. Hakuna mapacha .

Katika hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo ndani ya halmashauri ha mji wa Tarime wamezaliwa watoto tisa kati yao wa kiume ni watano na wa kike ni wanne.

Muunguzi mwandamizi hospitali ya wilaya ya Tarime , Mary Wilson amesema watoto hao wamezaliwa usiku wa Desemba, 24, 2025 . Kati yao Wavulana ni watano na wasichana ni wanne.

Amesema watoto wote wapo salama, watoto saba wamezaliwa kwa njia ya kawaida, na wawili kwa njia ya upasuaji .

No comments