HEADER AD

HEADER AD

RC MTAKA ATAMANI WATANZANIA MACHO YAO YAMULIKE FURSA VIJIJINI


>> Asema wakati wewe unasema kijijini kuna wachawi wageni wao wanaona fursa vijijini na kuwekeza

Na Mwandishi, Wetu Njombe

MKUU wa mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewahimiza watanzania kurejea Vijijini kwao kuwekeza kwa kile alichosema kwamba Vijijini kuna fursa, endapo zikitumika vizuri zitakuza uchumi kwa jamii za Vijijini na Taifa kwa ujumla.

Amewashangaa wanaoshindwa kurejea kijijini kwao kwa madai kwamba kijijini kuna uchawi lakini wageni wanapofika Vijijini huona fursa na kuwekeza.

" Wewe kijijini kwenu unaona uchawi lakini mchina anaona fursa kijijini. Mzaliwa anaona uchawi kijijini kwao , mgeni anaona fursa kijijini .

" Kuna mtu anatoka kijijini anasema kijijini ni wachawi hawezi kujenga nyumba wala kupeleka watoto wake. Lakini mchina yeye anaona fursa kwenye hicho Kijiji " amesema RC Mtaka.

RC Mtaka amesema kama kila mtanzania akiona Kijiji chake ni fursa matamanio ya Rais Dkt. Samia Suluhu kuwa na viwanda kwenye vijiji inawezekana .

" Umesoma hawakukuroga , umemaliza shule ukaenda chuo hawakukuroga ila ukianza safari ya mafanikio kule kijijini unasema ni wachawi wakubwa.

" Mke wako nae uliyemuoa kule unaona akienda kijijini atarogwa, watoto utakaowazaa ukienda kijijini watarogwa" amesema .

Ameongeza kusema, imefika wakati watu wanakwenda kijijini kwao pale wanapofiwa na kusema kwamba kama huo ndio mtazamo wa watanzania basi watu wa mataifa ndio watakaosaidia kuchemsha vijiji kupitia fursa mbalimbali.

" Watu wengi wanakwenda kijijini kwao wakati kafiwa . Kama ndio mtazamo wetu sisi watanzania kuwa Vijijini kwetu kuna uchawi basi ngoja watu wa mataifa mengine waje kutusaidia kuchemsha vijiji.

"Lakini kama sisi tukiona vijijini kwetu kuna fursa basi hakuna atakayekuja kuchemsha kwasababu tutajenga uchumi kwenye mikono yetu maana kule ni kwetu. " Amesema RC Mtaka.

Amewataka watanzania kutochagua maeneo ya uwekezaji kwani wapo wageni wanatumia gharama kubwa za usafiri kuja kuwekeza Tanzania.

" Unasema nitafutie shamba karibu na barabara , lakini mtu ambaye yupo Canada anahitaji shamba kijijini kwenu anatembea masaa 15 kuja Tanzania anatafuta shamba ,wewe wa hapo hapo unasema unatafuta shamba mjini hutaki shamba la mbali .

" Wewe kijijini kwako unaona fursa au unaona uchawi ?, wewe kwenu huko unakotokea unaona nini? " anauliza RC Mtaka.

No comments