HEADER AD

HEADER AD

KESI YA MAUAJI YA RHODA JONATHANI YAPIGWA KALENDA HADI MACHI 17


Na Mwandishi Wetu , Musoma

KESI ya mauaji inayowakabili washtakiwa watatu Mwita Maginga( 47) mkazi wa Tarime,  Marco Maginga (45) ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi jijini Mbeya na Simon Ruhinda (55) ambaye ni muhudumu  wa ofisi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara yapigwa karenda hadi Machi, 17 2026 .

Hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya Hakimu mkazi  Musoma, Eugenia Rujwahuka, akizungumza mahakamani hapo Machi, 03, 2026 amesema kesi hiyo iliyokuja kwa ajili ya kutajwa itatajwa tena Machi, 17, 2026.

" Wakili shida ni nini upelelezi bado tangu mwezi Desemba mwaka jana . Mnasema mna siku 90 za upelelezi " aliuliza hakimu.

Wakili wa Jamhuri Matha Mbosori , ameiambia mahakama hiyo kuwa upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea haujakamilika .

" Hii kesi inahusisha  upelelezi wa kina. Mhe. Hakimu naomba itajwe tarehe nyingine , upelelezi wa kina bado unaendelea haujakamilika " amesema Wakili Matha.

Washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya Rhoda Jonathani mkazi wa Kitongoji cha Burunga , Kata ya Uwanja wa Ndege wilayani Serengeti, mkoa wa Mara aliyekuwa mke wa Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA), mkoani Kagera, Mhandisi Wilson Charles .

     Askari wa Jeshi la Polisi wakiwapeleka mahakamani Mwita Maginga( 47) mkazi wa Tarime ( wa pili kushoto),  Marco Maginga (45) ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi jijini Mbeya (aliyevaa jaketi jeusi ) na Simon Ruhinda (55)  (aliyevaa sweta) ambaye ni muhudumu  wa ofisi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa  hilo siku ya alhamisi, tarehe ,23, Oktoba, 2025 majira ya kati ya saa moja na saa mbili usiku nyumbani kwa marehemu.

Kwa mara ya kwanza mtuhumiwa wa kwanza na wa pili walifikishwa katika  mahakama hiyo Desemba 12, 2025 na kufunguliwa shauri lenye namba 23/12/2025 kabla ya mtuhumiwa wa tatu kuunganishwa na wenzake Februari 3, 2026.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo  kinyume cha sheria za kanuni ya adhabu kifungu cha 196 na 197 ambapo wote wamerudishwa rumande kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana sambamba na mahakama hiyo ya hakimu mkazi kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.

>>Rejea  

Habari zilizopita za tukio hili zimeripotiwa katika chombo hiki cha habari , Februari, 17,2026 iliripotiwa habari isemayo ' KESI YA MAUAJI YA RHODA JONATHAN YAPIGWA KALENDA HADI MACHI 3.

Februari,03,2026, iliripotiwa habari yenye kichwa cha habari ' MUHUDUMU OFISI YA DED SERENGETI AUNGANISHWA KESI YA MAUAJI YA RHODA JONATHAN.

Januari, 05, 2026 iliripotiwa habari isemayo , KESI YA RHODA YAAHAIRISHWA HADI JANUARI, 19, UPANDE WA MASHTAKA HAWAKUFIKA MAHAKAMANI.

Desemba, 23, 2025 iliripotiwa  kichwa cha habari kisemacho ' MENEJA TARURA ALIYEKUWA AMESHIKILIWA POLISI KWA TUHUMA ZA MAUAJI AACHIWA, WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI'
 
Oktoba, 26,2025 iliripotiwa habari yenye kichwa cha habari 'MKE WA MENEJA TARURA AUAWA KWA KUKATWAKATWA MAPANGA SERENGETI. Oktoba, 26,2025 ikiripotiwa habari ' WAMUOMBA RAIS SAMIA, SERIKALI YA MARA KUWASAKA NA KUWAWAJIBISHA WALIOMUUA MKE WA MENEJA TARURA'

Pia Oktoba, 27, 2025 chombo hiki cha habari kiliripoti habari ' FIDIA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE SERENGETI HUWENDA IKAWA CHANZO CHA KUONDOA MAISHA YA MKE WA MENEJA TARURA'.

Oktoba 28,2025 ikiripotiwa habari ' MWILI WA RHODA ALIYEUAWA KWA MAPANGA WAENDELEA KUSOTA MOCHWARI, NDUGU WAGOMA KUZIKA. Novemba, 7,2025 iliripotiwa habari ' SERIKALI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WALIOHUSIKA MAUAJI YA MKE WA MENEJA TARURA'.


No comments