TAASISI YA ELIMU YATAKIWA KUENDELEA KUIMARISHA UFUATILIAJI MITAALA ILIYOBORESHWA
SERIKALI imeitaka Taasisi ya Elimu Tanzania kuendelea kuimarisha ufuatiliaji wa tathimini ya utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa ili kuleta matokeo chanya katika jamii.
Hayo yamesemwa tarehe 4/3/2026 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia . Wanu Hafidh Ameir alipofanya ziara ya siku moja katika taasisi hiyo ili kupata uelewa wa majukumu mbalimbali yanayofanywa na Taasisi katika kuchangia ukuaji wa Sekta ya Elimu nchini.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia . Wanu Hafidh Ameir.“Nashukuru kwa taarifa yenu ya utakelezaji wa majukumu mbalimbali ambayo inatoa picha halisi ya kazi kubwa inayofanywa TET.
" Nawaomba muimarishe kufanya tathimini ya utekelezaji wa mitaala iliyoboreshwa ili kama kuna changamoto ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka.” Amesema Wanu.
Amepongeza juhudi za utekeleaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 (Toleo la 2023) na mitaala iliyoboreshwa mwaka 2023 kwa vitendo, na kusema kuwa, inaonesha dhamira ya dhati katika kuimarisha ubora na mwelekeo wa elimu nchini.
Pia, Wanu ameipongeza TET kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwaomba kuendelea kufanya kazi kwa weledi na uzalendo, hususan katika kuboresha maudhui ya ujifunzaji kwa watoto wadogo kupitia katuni zenye maadili na tamaduni za Kitanzania.
Akieleza majukumu yanayotekelezwa na TET, Mkurugenzi Mkuu Dkt. Aneth Komba amesema TET kwa kushirikiana na wadau wa elimu, inaendelea kufanya tafiti mbalimbali za elimu zitakazosaidia kutatua changamoto mbalimbali katika eneo la ufundishaji na ujifunzaji.
Pia Dkt. Komba ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha za kutosha na kwa wakati zinazosaidia katika eneo la uandishi wa vitabu, uchapaji na usambazaji katika shule zote nchini.
.jpg)



Post a Comment