HEADER AD

HEADER AD

HAYA NI MAPENZI GANI

HAYA ni mapenzi gani,` wenzangu nijulisheni,

Majibu nipatieni, nami nipate baini,

Wabara na visiwani wasiwasi nitoeni,

Haya ni mapenzi gani ya kutumia mkono.


Faida yake ni nini, mkiweza nijuzeni,

Bado nipo mashakani, mbele sioni jamani,

Yawahusu watu gani, au ni jinsia gani,

Haya ni mapenzi gani ya kutumia mkono.


Leo nitafarijika, majibu kuyasikia,

Nitafurahi hakika, kwa hilo nikilijua,

Sitokuwa na mashaka, jibu mkinipatia,

Haya ni mapenzi gani ya kutumia mkono.


Siku moja nilikaa, pale kwetu kijiweni,

Stori nikasikia, nenda tumia sabuni,

Nikaanza fikiria, sabuni ni kitu gani,

Haya ni mapenzi gani ya kutumia mkono.


Wajuvi nijulisheni, kujua ninatamani,

Msiniache njiani, wadau nakuombeni,

Nijibuni kwa mizani, majibu yenye yakini,

Haya ni mapenzi gani ya kutumia mkono.


Majibu nasubiria, nimefikia mwishoni,

Shairi ninalitoa, ninaliacha hewani,

Mengi ninatarajia, mazuri na ya thamani,

Haya ni mapenzi gani ya kutumia mkono.


Tamani nimefikia, vya watu usitamani,

Usije kuangamia, ukajitoa thamami,

Mke wangu nimeoa, wewe wasubiri nini,?

Mke wa mtu ni sumu usiweke mazoea.

Mtunzi Sir Dody.

S. L. P, 8387,

Simu. 0671159555

Moshi, Kilimanjaro.

Mudio Islami Seminary

No comments